Skip to main content

Posts

KICHOMI

  Kichomi   ni moja ya dalili za ugonjwa moyo. Kupatwa kichomi mara moja moja si vibaya. Ukipatwa muda mrefu au kila wakati ; basi, chunguza zaidi. Kichomi husababishwa au kinaweza kuwa. Dalili ya matatizo ya tumbo lenye asidi (acid) kuzidi Dalili za ugonjwa wa moyo uitwao Ischemic Jambo la kuangalia ni je? Unashikwa kichomi ukiwa unatembea? Umeinama au umelala Ukishakula chakula Kama unapatwa kichomi wakati ukitembea au ukishafanya mazoezi makali ina maana kuna tatizo la damu kuingia sawasawa au kuzunguka (circulation) katika moyo. Kama unapatwa kichomi baada ya kula ina maana kuna tatizo katika chakula unachokula. Je mlo wako una acid(uchachu) sana? Je, unakula vyakula vyenye pilipili na binzari(spices) kwa wingi sana? Kama una kula sana vyakula vyenye asidi ina maana tumbo lako halimeng’enyui sawasawa linachoka. Kawaida binadamu unabidi kubadili badili ulaji. Usirudie vitu fulani fulani kila siku. Mathalan usiweke pilipili katika kila mlo. Tatizo ji...

FIBROID

Fibroid ni uvimbe ambao hutokea kwenye tumbo la kizazi ambao huu uvimbe unaweza kuwa ndani ya kizazi(ukutani mwa kizazi) au ndani ya nyama ya kizazi na nje kwenye ukuta wa kizazi. Kuna aina kuuzifuatazo za fibroids:  1.Submucosal fibroids(ndani ya kizazi)  2.Intramural fibroid(ndani ya nyama za kizazi)  3. Subserosal(nje ya kizazi).  Watu wafuatao wako hatarini ya kupata ugonjwa huu fibroids  1.Mwanamke ambae hajawahi kupata mtoto mpaka umri mkubwa  2.Miaka kuanzia kubarehe mpaka hedhi kukoma  3.Kurithi  4.Unene  5.Kuingia hedhi mapema Fibroids sio kansa ni uvimbe wa kawaida tu ambao unakua kwa kutegemea kichocheo cha estrogen hormone ndio maana kuanzia kubarehe mpaka kukoma kwa hedhi ndio wako hatarini. Na mara nyingi uvimbe huu waga unaongezeka kukua sana hasa wakati wa ujauzito kwani vichocheo hivi huongezeka wakati huu kulinda makazi ya mtoto. Ni watu waliofikia kikomo cha hedhi hawapati fibroids au kitaalam leomyoma....

UTATIZO LA UGUMBA KWA WANAWAKE

Ugumba kwa mwanamke ni tatizo la mwanamke kushindwa kushika mimba licha ya kushiriki kufanya mapenzi na mwanamume bila kutumia kinga. Tatizo la kutoshika mimba kwa kipindi angalau mwaka mmoja huku mwanamke huyo akishiriki kikamilifu ufanyaji mapenzi na mwanamume huitwa ugumba (Sterility). Ugumba kwa mwanamke (Sterility) sio sawa au haina maana sawa na tatizo la mwanamke kutojisikia au kutokuwa na hisia za kufanya mapenzi yaani ‘Frigidity’. Zipo sababu nyingi zinazoweza kufanya mwanamke awe mgumba. Mwanamume pia anaweza kuwa chanzo cha ugumba kwa maana kwamba hana uwezo wa kutungisha mimba. Hivyo,ndio kusema mwanaume kamwe hapaswi kumlaumu mwanamke anayeshirikiana naye kimapenzi kuwa ndiye ‘mgumba’ wakati mwanamume na mwanamke kwa pamoja wana asilimia sawa za kuwa chanzo cha ugumba. Ndio maana mwanamume na mwanamke wanapooana na wakashiriki ngono kikamilifu kwa kipindi cha mwaka mmoja, lakini hakuna dalili za mwanamke kuwa mjamzito, basi wote wawili wanapas...

MAKATAZO YA MAMBO YAFUATAYO KWA AFYA YAKO.

1. Usinywe maji ya moto baada ya kula chakula. 2. Usinywe maji ya baridi. 3. Usile vitunguu maji na kitunguu thaum kwa pamoja. 4. Usile kitu kikali halafu hapo hapo ukanywa maziwa ni hatari. 5. Usile mayai na maziwa kwa pamoja ni hatari sana. 6. Usile samaki na mayai inaweza sababisha madhara ya ukoma ugonjwa wa kufura viungo. 7. Usile baadae ukaoga hii ni hatari inaweza kukuletea tumbo la.mshipa bora ni uoge ndio ule. 8. Usifanye hijama (kuundama) ukiwa na mkojo inasababisha maradhi ya kibofu cha mkojo. Kwa tiba za maradhi mbalimbali wasiliana nami.

KUZUIA KUTAPIKA

chukua ubani mustaka na karafuu zote zikiwa unga na ujazo sawa na utie kijiko kimoja cha mchanganyiko huo kwenye maji glass moja na unywe.

U T I ( URINARY TRACT INFECTION)

NINI MAANA YA U.T.I? U.T.I ni kifupi cha maneno ya kiingereza: ‘Urinary tract infections’, ni maambukizi ya bakteria katika njia ya mkojo. Husababishwa na bacteria aina ya clamydia tracomatis,  Ni moja ya ugonjwa unaowakumba sana wanawake kwa sehemu kubwa ingawa hata wanaume pia wanapatwa na ugonjwa huu. CHANZO CHA UGONJWA. →Kushikilia mkojo kwa muda mrefu →Kukojoa kwenye maji machafu →Mawe kwenye figo. →Kuongezeka ukubwa wa kibofu cha mkojo. →Upungufu wa maji mwilini →Ajari katika uti wa mgongo →Maji maji na uchafu katika sehemu za siri. →Kufanya ngono na muathilika wa U.T.I →Kujisaidia sana kwenye vyoo vya uma, DALILI ZA U.T.I →kujisikia homa kali. →Kuhisi baridi kali, →maumivu nyuma ya mgongo →Kukojoa mara kwa mara →Mikojo kukutoka pasipo kutaka →Harufu nzito au mbaya ya mkojo →Hali ya kusikia kuungua wakati wa kukojoa →Kupatwa ghafla na hitaji la kutaka kukojoa Mkojo kutoka wa rangi ya njano. →Maumivu kwenye kibofu cha mkojo n...

TATIZO LA UPUNGUFU WA DAMU ( ANAEMIA ) KWA MAMA MJAMZITO.

Upungufu wa damu husababishwa na nini?. Upungufiu wa damu husababishwa na ukosefu wa madni chuma mwilini (Iron). Mwili unaitaji madini chuma kwa wingi kwa ajili ya kutengeneza chembe hai nyekundu  za damu (red blood cell). Unapokuwa mjamzito kiwngo cha madini chuma (Iron) yanayotakiwa mwilini huongezeka kutoka 18 milligram kwa siku mpaka 27 milligram kwa siku. hii ni kutokana na mwili kuhitaji damu nying kwa ajili ya kufanya kazi mbalimbali zinazoongezeka mwilini kwa ajili ya kusapoti ukuaji wa mtoto. Damu ni muhimu sana kwa mama mjamzito. Hivyo basi jitahid kula yakula vyenye kuongeza Damu. Vyakula vinavyoongeza Damu vimegawika katika makund mawili Heme Iron. hivi ni vyakula ambavyo mwili huweza kuichukua kirahis Iron yake navyo ni Nyama,Samaki,Kuku,Maini na Dagaa. Pia kuna Non Heme. hivi ni vyakula ambavyo vina Iron ya kutosha ila mwil hauwezi kuichukua kirahis hivyo basi unapokula vyakula hivyo jitahid kula vyakula vyenye vitamin C kama Mac...