VIDONDA VYA TUMBO NI NINI ?. Vidonda vya tumbo ni matokeo ya kuharibika kwa uteute wa ndani ya ukuta wa tumbo la Chakula au ndani ya utumbo mdogo wa Chakula na matokeo yake ni ukuta wa tumbo kugusana na tindikali iliyoko tumboni ambayo ni kali sana. NINI HUSABABISHA vidonda vya tumbo husababishwa na maambukizi ya bacteria waitwao HELICOBACTER PYLORI, aidha matumizi ya baadhi ya dawa za kutuliza maumivu za jamii ya Nonsteroids anti inflammatory drugs huweza kusababisha uwezekano wa kupata ugonjwa huu, Vidonda vya tumbo vinaweza kujitokeza katika utumbo mdogo na katika tumbo la Chakula na pia ni Mara chache huweza kujitokeza katika koo la Chakula ambapo hapakukusudiwa kustahimili tindikali ya tumbo. Kuna Aina tatu za Vidonda vya Tumbo(peptic ulcers). 1.GASTRIC ULCERS. Hivi ni vidonda vinavyotokea katika mfumo wa Chakula yani tumboni. 2.DUODENAL ULCERS. Hivi ni vidonda vinavyotokea katika utumbo mdogo. 3.OESOPHAGEALS ULCERS. Hivi ni vidonda vinavyotokea katika k...