Skip to main content

Posts

Showing posts from February 14, 2018

SARATANI YA NGOZI (MELANOMA )

Melanoma ni saratani hatari sana kwa maisha ya mwanadamu. Saratani hii huwapata watu wachache lakini inapotokea mtu akapata saratani hii basi maisha yake huwa hatarini. Saratani hii si rahisi kugundulika ikilinganishwa na saratani nyingine za ngozi. Siyo tu kwamba saratani hii ni ngumu kidogo kutambulika bali pia husambaa haraka zaidi kuliko saratani nyingine za ngozi. Melanoma huweza kusambaa na kushambulia viungo vingine zaidi ya ngozi kama mifupa na ubongo. Inapofikia hatua hii saratani hii huwa ngumu sana kutibika. Ni nani wanaoweza kupata kansa ya ngozi? Mbali na watu ambao wamewahi kupigwa na jua kwa muda mrefu sana, au wale wanaojianika juani kwa vipindi virefu, wale walio na ngozi nyeupe, nywele na macho ya rangi hafifu, wenye mabaka na madoadoa, na wale ambao mtu fulani katika familia yao amekuwa na ugonjwa huo, wanaweza kuupata. Watu weupe hupatwa na kansa ya ngozi zaidi kuliko watu weusi. Lakini je, hii inamaanisha kwamba kadiri ngozi yako inavyounguzwa na jua na kuwa n...