KUNG'ARISHA USO NA KUTOA MADOA DOA USONI. Chukua uwatu usage mpaka uwe laini sana. Kisha utaosha uso wako kwa maji vuguvugu na ukaushe kabisa. Baada ya hapo utachukua unga wa uwatu kijiko kimoja na utachanganya maji ya kawaida ama maji ya waridi mpaka iwe marham/rojo (paste) na utajipaka usoni na kuiacha ikauke kwa mda wa dakika 10-15 na utaosha na kupaka mafuta yako. NB Hakikisha zoezi hili unalifanya mara tatu kwa wiki kwa ajili ya matokeo mazuri. Na ni bora ukifanya usiku kabla hujalala.