Moyo kupanuka au kuwa mkubwa ni tatizo ambalo huathiri utendaji wa mfumo wa usambazaji damu mwilini. Ni hali inayosababishwa na ukinzani wa moyo jinsi unavyotoa na kuingiza damu katika mishipa ya moyo na kuelekea sehemu mbalimbali za mwili. Moyo kupanuka kutokana na kutokana na mazingira ya kusukuma damu kwa nguvu ya ziada tofauti na kawaida, hivyo kusababisha misuli ya moyo kuharibika. Wakati mwingine moyo hutanuka bila sababu zinazojulikana moja kwa moja. Pia, wakati mwingine moyo unaweza kutanuka kwa kipindi kifupi kutokana na mgandamizo kwenye mwili wako mfano ujauzito. Hali nyingine ni tatizo la moyo ulilozaliwa nalo, kuharibika kwa moyo kutokana na mshtuko wa moyo, kudhoofu kwa misuli ya moyo au moyo kutodunda kwa mpangilio. Mazingira hayo huweza kusababisha moyo kutanuka. Hali zingine za kiafya zinazohusiana na moyo kutanuka ni kama zifuatazo: Kupanda kwa shinikizo la damu Hali hii husababisha moyo kusukuma damu kwa nguvu zaidi ili kuifikisha sehe...