Skip to main content

Posts

Showing posts from August 31, 2017

KUZUIA KUTAPIKA

chukua ubani mustaka na karafuu zote zikiwa unga na ujazo sawa na utie kijiko kimoja cha mchanganyiko huo kwenye maji glass moja na unywe.

U T I ( URINARY TRACT INFECTION)

NINI MAANA YA U.T.I? U.T.I ni kifupi cha maneno ya kiingereza: ‘Urinary tract infections’, ni maambukizi ya bakteria katika njia ya mkojo. Husababishwa na bacteria aina ya clamydia tracomatis,  Ni moja ya ugonjwa unaowakumba sana wanawake kwa sehemu kubwa ingawa hata wanaume pia wanapatwa na ugonjwa huu. CHANZO CHA UGONJWA. →Kushikilia mkojo kwa muda mrefu →Kukojoa kwenye maji machafu →Mawe kwenye figo. →Kuongezeka ukubwa wa kibofu cha mkojo. →Upungufu wa maji mwilini →Ajari katika uti wa mgongo →Maji maji na uchafu katika sehemu za siri. →Kufanya ngono na muathilika wa U.T.I →Kujisaidia sana kwenye vyoo vya uma, DALILI ZA U.T.I →kujisikia homa kali. →Kuhisi baridi kali, →maumivu nyuma ya mgongo →Kukojoa mara kwa mara →Mikojo kukutoka pasipo kutaka →Harufu nzito au mbaya ya mkojo →Hali ya kusikia kuungua wakati wa kukojoa →Kupatwa ghafla na hitaji la kutaka kukojoa Mkojo kutoka wa rangi ya njano. →Maumivu kwenye kibofu cha mkojo n...

TATIZO LA UPUNGUFU WA DAMU ( ANAEMIA ) KWA MAMA MJAMZITO.

Upungufu wa damu husababishwa na nini?. Upungufiu wa damu husababishwa na ukosefu wa madni chuma mwilini (Iron). Mwili unaitaji madini chuma kwa wingi kwa ajili ya kutengeneza chembe hai nyekundu  za damu (red blood cell). Unapokuwa mjamzito kiwngo cha madini chuma (Iron) yanayotakiwa mwilini huongezeka kutoka 18 milligram kwa siku mpaka 27 milligram kwa siku. hii ni kutokana na mwili kuhitaji damu nying kwa ajili ya kufanya kazi mbalimbali zinazoongezeka mwilini kwa ajili ya kusapoti ukuaji wa mtoto. Damu ni muhimu sana kwa mama mjamzito. Hivyo basi jitahid kula yakula vyenye kuongeza Damu. Vyakula vinavyoongeza Damu vimegawika katika makund mawili Heme Iron. hivi ni vyakula ambavyo mwili huweza kuichukua kirahis Iron yake navyo ni Nyama,Samaki,Kuku,Maini na Dagaa. Pia kuna Non Heme. hivi ni vyakula ambavyo vina Iron ya kutosha ila mwil hauwezi kuichukua kirahis hivyo basi unapokula vyakula hivyo jitahid kula vyakula vyenye vitamin C kama Mac...

KISUKARI

kisukari au bolisukari (jina la kitaalamu:  diabetes mellitus ) ni ugonjwa unaoonyesha viwango vikubwa vya glukosi katika damu. Sababu yake ni uhaba wa homoni ya insulini mwiliniau upungufu wa uwezo wa mwili wa kukubali insulini. Dalili za kisukari ni kukojoa kupita kiasi cha kawaida kiu kikubwa kuona vibaya na matatizo ya macho hadi kuwa kipofu kuchoka haraka vidonda vinavyopoa polepole mno hasa kwenye miguu hadi kupotea viungo Watu wachache huzaliwa na uhaba wa insulini. Walio wengi wana udhaifu fulani unaokuwa hatari kutokana na aina za vyakula na maisha ya kila siku. Kutumia sukari nyingi pamoja na mafuta mengi katika chakula na vivywaji, kukosa mazoezi ya mwili (kwa watu wenye kazi ofisini), kunywa pombe nyingi na kuvuta sigara huongeza hatari ya kushika kisukari kuanzia baada ya miaka ya ujana. sababu ya kisukari - uzito mwingi mwi...

UGONJWA WA RETINA UNAOSABABISHWA NA KISUKARI

Jicho ni kiungo ambacho binadamu anapaswa kuwa makini kukilinda maana kuwapo kwake kunasaidia viungo kutenda kazi vyema. idadi ya wagonjwa wengi wakisukari nchini na duniani inazidi kuongezeka. Ugonjwa huu wa macho huwapata watu wenye kisukari cha muda mrefu. Kuwapo kwa ugonjwa wa kisukari husababisha kuharibika kwa retina. Hii ni sehemu ya nyuma ya jicho ambayo inaundwa kwa utando wa neva ama mishipa ya fahamu. Mishipa hii ya fahamu ni muhimu sana katika kumuwezesha mtu kuona. Ndio inayopokea taswira ya vitu na kuipeleka katika ubongo kwa ajili ya tafsiri. Kuathirika kwa neva hizi ni tatizo la hatari kwa uwezo wa jicho kuona kwani inaweza kusababisha kuwa na uwezo mdogo wa kutambua taswira ya vitu. Hali hii isipotibiwa mapema, husababisha ulemavu wa kudumu. Kisukari ni ugonjwa unaoingilia uwezo wa mwili kutumia na kuhifadhi sukari mwilini. Hii husababisha madhara makubwa mwilini. Sukari ndio nishati inayotegemewa na mwili katika kuendesha shughuli mbalimbali. Kwa...