Leo nataka kupeana faida ndogo kuhusu mafuta yaliyochanganywa na *BUNSAJI.*mafuta haya hufaa sana kwa :- - kichwa kilicho na harara ukipaka kichwani. - mafuta hayo huwafaa sana watu ambao hawapati usingizi wakipaka kichwani. - mafuta hayo hurutubisha ubongo ukipaka kichwani. - hufaa sana kwa watu wenye uyabisi na kupasuka pasuka ( dandruff ) ukipaka kichwani. - hufaa sana kwa mtu anaejikuna sana kichwani. *NAMNA YA KUYATENGENEZA.* chukua bunsaji kisha iponde iwe unga kisha iroweke katika maji unayotaka kuyachemsha masaa 12, baada ya hapo utaichemsha sana mpaka ibaki sawa na mafuta yako unayotaka kuchanganyia kama ni ya nazi, zaituni ama yeyote yale. Kama itakuwa mafuta yako ni nusu lita hakikisha umeichemsha bunsaji mpaka ikafika nusu lita nayo, kisha changanya pamoja baada ya kuichuja na uweke jikoni ichemke mpaka maji yote ya bunsaji yamekauka na kubaki mafuta pekee. Hapo sasa itakuwa tayari kwa matumizi. Kwa ushauri/tiba ya maradhi mbalimbali wasiliana nami.