Skip to main content

ALMONDS/LOZI


leo ndugu zangu nataka kuzungumzia faidia cheche zitokanazo na tunda hili.
watu wengi wamelichukulia tunda hili huliwa na watu wenye maradhi ama wenye hela zao. Ila kwa ushauri nawaomba tukumbatie tunda hili kwa wingi maana lina faida nyingi sana. Hizi ni baadhi ya faida ya tunda hili:-

- husafisha tumbo.
- huongeza maziwa mengi kwa wanyonyeshaji.
- kusaidia sana kwa wenye maradhi ya mishipa/nerves.
- husaidia sana kwa watu wenye maradhi ya kibofu cha mkojo.
- lozi ni nzuri sana kwa mtu mwenye maradhi ya figo.
- ni nzuri sana kwa wenye maradhi ya kisukari.
- hufungua njia za mkojo.
- lozi hutia nguvu ubongo hasa kwa wenye kusahau sahau na udhaifu wa kumbukumbu.
- mafuta yake ni mazuri kwa mtu mwenye maradhi ya ngozi hutibu.
- mafuta yake ni mazuri kwa mtu aliepooza, hutibu.
- mafuta yake ni mazuri kwa mtu aliyechomeka ngozi, hutibu.
- lozi husaidia kwa mtu mwenye uchache wa mbegu za kiume.

NB tunda hili linatibu maradhi mengi sana.

Kwa ushauri/tiba wasiliana nami
karibuni mombasa kenya

Comments

Popular posts from this blog

MDUDU WA KIDOLE

Huu ni ugonjwa unaoathiri vidole vya miguu na mikono, sana sana unaathiri mikononi nadra sana mguuni.tatizo hili lisipotibiwa kwa mapema linaweza hata kufanya kidole kikakatika. Zifuatazo ni tiba za kutibu maradhi Haya :-  Njia ya kwanza Chukua mbaazi kidogo kisha ziroweke kwenye maji kwa mda mpaka zilainike, halafu utaziweka kwenye kinu na kuzitwanga mpaka zilainike, ukikosa kinu tumia kitu chochote cha kusagia ili tu ziwelaini sana. Halafu utachukua dawa hiyo na kupaka kwenye sehemu iliyoathirika na kufunga kwa kitambaa usiku mzima. Na ukiamka itakuwa imechuja uchafu wote na kufanya sehemu iliyoathirika kupona, ikiwa bado toa hiyo dawa na kufunga nyengine. Kwa uwezo was ALLAH dawa hii utapona na no mujarrab. Njia ya pili Tiba hii ni kwa mdudu anaeanza sasa kabla hajaiva na kuwa rangi ya njano. Chukua kitunguu thaum kisage kiwe laini na upake sehemu iliyoathirika kwa mda was masaa 12 kisha toa na kupaka nyengine mpaka utakapo pata nafuu. Mpemba herbal +254732917064...

UTOSI KUINGIA NDANI KWA MTOTO MCHANGA.

chukua manjano mbichi iponde iwe laini sana, kisha chukua pamba na uiweke ile dawa, kisha muekee mtoto mchanga aliena tatizo hilo utosini. In shaa allah utosi utarudi sawa. Utafanya hivyo kwa siku mara moja mpaka tatizo litakapokwisha.

HEDHI KUTOKA KIDOGO KIDOGO.

hii Mara nyingi inasababishwa na mambo kadhaa ikiwemo hormone imbalance, kutumia Dawa za family planning na matatizo mbali mbali yanayompata mwanamke ndani ya mwezi uliopita. Kwa ushauri mwanamke anatakikana spate vipimo ama amuone daktari kwa vipimo na ushauri zaidi. Kama itakuwa sio kwababu ya mimba basi mgonjwa anatakikana kutumia Dawa zifuatazo ilikufanya hedhi itoke kama kawaida. 1. Chukua mvuje na pilipili manga chemsha pomoja na anywe kikombe cha kahawa kutwa Mara tatu. 2. Chukua manemane ichemshe na mgonjwa anywe asubuhi kabla ya kula kitu kwa mda wa siku tatu. Kwa Dawa na ushauri wa magonjwa mengine wasiliana nami +254732917064.