Skip to main content

Posts

Showing posts from October 3, 2017

HIATUS HERNIA (NGIRI YA KIFUA)

Hiatus Hernia   ni tundu linalotokea baada ya sehemu ya juu ya mfuko wa kuhifadhia chakula (tumbo) kuingia kwenye sehemu ya kifua kupitia uwazi unaojulikana kama   esophageal hiatus . Kwa kawaida uwazi huu   (esophageal hiatus)   hupitisha mrija wa chakula kwenda kwenye tumbo yaani   esophagus   na si utumbo. Mara nyingi, tatizo hili huonekana kwa takribani ya 60% ya watu wenye umri wa miaka 50 na kuendelea, ingawa pia linaweza kuwapata wale walio na umri wa chini ya huo. Kuna aina mbili kuu za hiatus hernia Sliding type :  Kama jina lake linavyomaanisha, aina hii hutokea iwapo sehemu ya juu ya utumbo inaposukumwa juu na kuingia kwenye upenyo wa  esophagus hiatus  baada ya kutokea kwa ongezeko la presha katika maeneo ya tumbo  (increased pressure in the abdominal cavity)  na kurudi kama kawaida wakati presha inapopungua. Fixing type : Aina hii hutokea iwapo sehemu ya juu ya utumbo inapoku...