Skip to main content

Posts

Showing posts from October 16, 2017

DEGEDEGE

Degedege Ni Nini ? Ni hali ya ghafla ya kutingishika kwa mwili mzima au miguu na mikono,ambayo husababishwa na kukakamaa kwa misuli ya mwili. Hali hii uhusishwa na magonjwa ya ubongo kama kifafa,vichocheo vya kwenye damu kama upungufu wa sukari(hypoglycemia), upungufu wa oxygen(hypoxia),kushuka kwa shinikizo la damu(hypotension) na maambukizi na homa ya degedege. Homa ni Nini ?. Ni hali ya kawaida ya mwili kushindwa kujikinga na maambukizi. Na kwa watoto hutokea pale joto la mwili linapokuwa zaidi ya nyuzi 38 za sentigredi. Homa ya Degedege Ni Nini ?. Ni degedege linalotokea kwa watoto ghafla likiambatana na homa kali iliyotokana na kuongezeka haraka kwa joto la mwili. Ugonjwa huu utokea kwa wastani wa asilimia nne (4%) ya watoto walio kati ya umri wa miezi sita na miaka mitano. Watoto wengi ambao hupatwa na ugonjwa huu huwa haiwapelekei baadae kuwa na matatizo ya kudumu kama kupata ugonjwa wa kifafa,niasilimia tatu (3%) tu ambao wanaweza baadae kupata ugonjwa w...