Skip to main content

DEGEDEGE

Degedege Ni Nini ?

Ni hali ya ghafla ya kutingishika kwa mwili mzima au miguu na mikono,ambayo husababishwa na kukakamaa kwa misuli ya mwili.


Hali hii uhusishwa na magonjwa ya ubongo kama kifafa,vichocheo vya kwenye damu kama upungufu wa sukari(hypoglycemia), upungufu wa oxygen(hypoxia),kushuka kwa shinikizo la damu(hypotension) na maambukizi na homa ya degedege.


Homa ni Nini ?.


Ni hali ya kawaida ya mwili kushindwa kujikinga na maambukizi.


Na kwa watoto hutokea pale joto la mwili linapokuwa zaidi ya nyuzi 38 za sentigredi.


Homa ya Degedege Ni Nini ?.

Ni degedege linalotokea kwa watoto ghafla likiambatana na homa kali iliyotokana na kuongezeka haraka kwa joto la mwili.

Ugonjwa huu utokea kwa wastani wa asilimia nne (4%) ya watoto walio kati ya umri wa miezi sita na miaka mitano.


Watoto wengi ambao hupatwa na ugonjwa huu huwa haiwapelekei baadae kuwa na matatizo ya kudumu kama kupata ugonjwa wa kifafa,niasilimia tatu (3%) tu ambao wanaweza baadae kupata ugonjwa wa kifafa.


Mmoja kati ya watoto watatu anbao wamewahi kuwa na homa ya degedege wanaweza wakapatwa tena na tatizo hili.


baadhi ya watoto wanaweza wasipatwe kabisa na tatizo hili au wakapatwa mara moja tu kwa maisha yao yote.


Lakini hauna jinsi ya kutabiri ni mtoto yupi ambaye anaweza kupatwa na shambulio hili.


Homa ya Degedege Hutokea kwa Watoto Gani ?.

Watoto wanaweza kurithi tabia hii ya kuumwa homa ya degedege kutoka kwa wazazi wao.


Kama mama au baba aliwahi kuumwa ugonjwa huu basi mtoto ana asilimia 10-20 zaidi ya kuumwa ugonjwa huu hukilinganisha na yule ambaye wazazi wake hawakuwai kuumwa ugonjwa huu.


Homa isababishwayo na maabukizi yoyote yale kama virus,bakteria na parasite.


Dalili za Homa ya Degedege ni Zipi ?.


Shambulio la ugonjwa huu likijitokeza mtoto uanza na kupotewa na fahamu na muda mfupi baadae mwili,miguu na mikono uanza kukakamaa na kurudisha kichwa nyuma,baada ya hayo miguu na mikono uanza kujitikisa.


Kushindwa kupumua na kutokwa na mapovu mdomoni.

Macho kugeukia nyuma na kuonekana kwa sehemu nyeupe ya jicho.

Shambulio huisha baada ya muda mfupi mara nyingi chini ya dakika tano


Baada ya shambulio mtoto hupitiwa na usingizi mzito kama takribani dakika 30 hadi saa nzima.


Akizinduka anaweza kushindwa hata kukutambua na akawa atamani kitu chochote kwa muda huo.


Nini cha Kufanya Mtoto anapopatwa na Shambulio.

Tulia na usichanganyikiwe.

Ondoa vitu vya hatari karibu na mtoto na muweke sehemu ya usalama kama sakafuni.

Usijaribu kuweka kitu chochote mdomoni kwa mtoto hata vidole vyako.

Angalia muda wa shambulio kuanza hadi litakapo isha ili umueleze daktari.

Baada ya shambulio kuisha mlaze mtoto kwa upande na usimuamshe muache apumzike.

Shambulio la homa ya degedege sio kifafa na mtoto hapati maumivu yoyote wakati wa shambulio kwa hiyo usimpe dawa yoyote ile.

Kwa tiba kamili wasiliana nasi.

Popular posts from this blog

MDUDU WA KIDOLE

Huu ni ugonjwa unaoathiri vidole vya miguu na mikono, sana sana unaathiri mikononi nadra sana mguuni.tatizo hili lisipotibiwa kwa mapema linaweza hata kufanya kidole kikakatika. Zifuatazo ni tiba za kutibu maradhi Haya :-  Njia ya kwanza Chukua mbaazi kidogo kisha ziroweke kwenye maji kwa mda mpaka zilainike, halafu utaziweka kwenye kinu na kuzitwanga mpaka zilainike, ukikosa kinu tumia kitu chochote cha kusagia ili tu ziwelaini sana. Halafu utachukua dawa hiyo na kupaka kwenye sehemu iliyoathirika na kufunga kwa kitambaa usiku mzima. Na ukiamka itakuwa imechuja uchafu wote na kufanya sehemu iliyoathirika kupona, ikiwa bado toa hiyo dawa na kufunga nyengine. Kwa uwezo was ALLAH dawa hii utapona na no mujarrab. Njia ya pili Tiba hii ni kwa mdudu anaeanza sasa kabla hajaiva na kuwa rangi ya njano. Chukua kitunguu thaum kisage kiwe laini na upake sehemu iliyoathirika kwa mda was masaa 12 kisha toa na kupaka nyengine mpaka utakapo pata nafuu. Mpemba herbal +254732917064...

UTOSI KUINGIA NDANI KWA MTOTO MCHANGA.

chukua manjano mbichi iponde iwe laini sana, kisha chukua pamba na uiweke ile dawa, kisha muekee mtoto mchanga aliena tatizo hilo utosini. In shaa allah utosi utarudi sawa. Utafanya hivyo kwa siku mara moja mpaka tatizo litakapokwisha.

HEDHI KUTOKA KIDOGO KIDOGO.

hii Mara nyingi inasababishwa na mambo kadhaa ikiwemo hormone imbalance, kutumia Dawa za family planning na matatizo mbali mbali yanayompata mwanamke ndani ya mwezi uliopita. Kwa ushauri mwanamke anatakikana spate vipimo ama amuone daktari kwa vipimo na ushauri zaidi. Kama itakuwa sio kwababu ya mimba basi mgonjwa anatakikana kutumia Dawa zifuatazo ilikufanya hedhi itoke kama kawaida. 1. Chukua mvuje na pilipili manga chemsha pomoja na anywe kikombe cha kahawa kutwa Mara tatu. 2. Chukua manemane ichemshe na mgonjwa anywe asubuhi kabla ya kula kitu kwa mda wa siku tatu. Kwa Dawa na ushauri wa magonjwa mengine wasiliana nami +254732917064.