Kwa undani kuhusu mabusha. Mabusha ni hali ya kujaa maji kwenye mfuko wa pumbu. Hali hii hutokea kunapokuwa na mkusanyiko wa maji kati ya tabaka mbili za utando unaozunguka korodani. Dalili za Mabusha. Katika hatua za awali, mabusha hayana dalili zozote (asymptomatic). Hata hivyo, baada ya muda fulani, mapumbu hujaa na uvimbe huweza kuonekana hata kwa nje. Kwa kadiri uvimbe unavyozidi kuongezeka, dalili zifuatazo zaweza kujitokeza pia; Muhusika kujihisi hali ya uzito na kuvuta sehemu za siri kutokana na kujaa na kuongezeka kwa uzito wa mapumbu. Mgonjwa huweza kujihisi hali ya usumbufu na kutojisikia vizuri maeneo ya kinena mpaka mgongoni. Kwa kawaida mabusha hayana maumivu yeyote. Hata hivyo, iwapo mgonjwa ataanza kujihisi maumivu, hiyo ni dalili ya kuwepo kwa uambukizi katika mshipa wa epididymis (acute epididymitis). Uvimbe huwa na tabia ya kupungua iwapo mgonjwa atakaa kitako na huongezeka pindi anaposimama. Iwapo mgonjwa atajisikia homa, kichefuche...