Skip to main content

PARACHICHI

Faida za parachichi.

Parachichi ni tunda ambalo mti wake hujulikana kisayansi kama Persea amerikana.

Tunda hili lina aminika kuwa na asili kutoka jimbo la Puebla,bara Amerika ya kusini kunako nchi ya
Mexico.

Lakini kutokana na faida nyingi kiafya zipatikanazo kwa ulaji wa tunda hili, tunda hili sasa hupatikana na kutumika kwa lishe sehemu nyingi duniani hususani barani Afrika.

Parachichi ni tunda la pekee
ukilinganisha na matunda mengine,
kimsingi matunda mengine huwa yana wanga( carbohydrate) kwa wingi,wakati parachichi lina aina ya mafuta ambayo yana faida kwa afya.

Parachichi katika tafiti nyingi
limeonekana kuwa na faida katika
afya ya moyo. Wagonjwa wa moyo
wamekuwa katika makatazo ya
kutumia aina ya mafuta ambayo
yamekuwa yakichangia kuongezeka
kwa lehemu katika damu(mafuta hayo kitaalam kama polysaturated fat ), na kuongeza matumizi ya mafuta yasiyoongeza lehemu katika damu (monosaturated fat ).

Parachichi ni chanzo kizuri cha mafuta yasiyoongeza lehemu katika damu.

Utafiti unaonyesha kuwa matumizi ya mafuta haya katika parachichi
hupunguza lehemu iliyo hatari
( kitaalam kama, Low density
lipoprotein ), na huchangia katika
ongezeko la lehemu isiyo hatari
( High density lipoprotein ).

Madini ya Potasiamu ni aina ambayo
huwa watu hawapati ya kutosha
kutoka katika vyakula. Parachichi lina kiwango kikubwa cha madini ya potassium kuliko ndizi. Tafiti
mbalimbali zimeonyesha kuwa
matumizi ya madini haya huambatana na kupungua kwa shinikizo la damu,

shinikizo la juu la damu laweza
kupelekea mtu kupata kiharusi,
shambulizi la moyo hata figo
kushindwa kufanya kazi.

Parachichi lina kiwango kikubwa cha fiba. Fiba ni kirutubisho kutoka katika vyakula vya jamii ya mimea, fiba huwa hazimeng’enywi tumboni lakini huwa zina umuhimu mkubwa sana, kama kusaidia kupunguza uzito wa mwili, kusaidia urekebishaji wa kiwango cha
sukari mwilini na kupunguza hatari ya kupata magonjwa mengi mwilini.

 Kuna aina fulani ya fiba ambazo huwa ni virutubisho kwa ajili ya bakteria wenye faida tumboni, hii huimarisha kinga ya mwili na kusaidia mwili kufanya kazi
katika kiwango kinachotakiwa.Kwa
kuwa parachichi lina kiwango kikubwa cha fiba, husaidia kuboresha mmeng’enyo na kupata choo katika hali ya kawaida.

Aina ya mafuta na virutubisho
tulivyoviona awali katika parachichi
vinasaidia afya ya ngozi yako.

Husaidia ngozi yako kutokuwa kavu
na kuwa na unyevu unaotakiwa na
kuifanya ngozi kuwa laini na yenye
afya.

Vitamini C husaidia katika kusaidia uponaji haraka wa ngozi na
kujijenga upya kwa seli za ngozi
zilizoharibika,husaidia kujenga elastini na collageni ambazo ni muhimu katika ngozi. Uwepo wa virutubisho viondoavyo sumu
( antioxidants) katika parachichi kama carotenoidi na vitamini E, hutusaidia kutukinga na
mionzi mikali ya jua, kwa hiyo huzuia makunyanzi katika ngozi na kuifanya ngozi yako kuwa na mwonekano mzuri wakati wote.

Tunda hili ni lishe bora kwa wale
wenye kisukari. Parachichi lina
kiwango kidogo cha sukari
ukilinganisha na matunda mengine.

Pia uwepo wa mafuta aina ya
‘monosaturated’ husaidia kuboresha
ufanyaji kazi wa homoni ya insulini,
katika urekebishaji wa kiwango cha
sukari mwilini.

Faida nyingine ni kuwa Vitamini C katika parachichi husaidia kuimarisha mishipa ya damu na kuboresha kinga ya mwili ambayo ni faida kubwa kwa wagonjwa wenye kisukari.

Faida katika afya ya uzazi ni dhahiri. Parachichi lina Vitamini E ambayo ni “antioxidant ” Potasiamu, Vitamini B6,Vitamini C ambazo hutusaidia kutukinga na magonjwa ya moyo hata yale ya kisukari.

Chochote kile kinachosaidia afya ya moyo pia husaidia afya ya uzazi.

Wanaume wenye magonjwa ya moyo na kisukari huwa na tatizo kubwa la upungufu wa nguvu za kiume.Parachichi pia limeonekana kuwa na faida nyingi katika kuboresha afya ya macho, viungo vya mwili na nyinginezo nyingi.

Popular posts from this blog

MDUDU WA KIDOLE

Huu ni ugonjwa unaoathiri vidole vya miguu na mikono, sana sana unaathiri mikononi nadra sana mguuni.tatizo hili lisipotibiwa kwa mapema linaweza hata kufanya kidole kikakatika. Zifuatazo ni tiba za kutibu maradhi Haya :-  Njia ya kwanza Chukua mbaazi kidogo kisha ziroweke kwenye maji kwa mda mpaka zilainike, halafu utaziweka kwenye kinu na kuzitwanga mpaka zilainike, ukikosa kinu tumia kitu chochote cha kusagia ili tu ziwelaini sana. Halafu utachukua dawa hiyo na kupaka kwenye sehemu iliyoathirika na kufunga kwa kitambaa usiku mzima. Na ukiamka itakuwa imechuja uchafu wote na kufanya sehemu iliyoathirika kupona, ikiwa bado toa hiyo dawa na kufunga nyengine. Kwa uwezo was ALLAH dawa hii utapona na no mujarrab. Njia ya pili Tiba hii ni kwa mdudu anaeanza sasa kabla hajaiva na kuwa rangi ya njano. Chukua kitunguu thaum kisage kiwe laini na upake sehemu iliyoathirika kwa mda was masaa 12 kisha toa na kupaka nyengine mpaka utakapo pata nafuu. Mpemba herbal +254732917064...

UTOSI KUINGIA NDANI KWA MTOTO MCHANGA.

chukua manjano mbichi iponde iwe laini sana, kisha chukua pamba na uiweke ile dawa, kisha muekee mtoto mchanga aliena tatizo hilo utosini. In shaa allah utosi utarudi sawa. Utafanya hivyo kwa siku mara moja mpaka tatizo litakapokwisha.

HEDHI KUTOKA KIDOGO KIDOGO.

hii Mara nyingi inasababishwa na mambo kadhaa ikiwemo hormone imbalance, kutumia Dawa za family planning na matatizo mbali mbali yanayompata mwanamke ndani ya mwezi uliopita. Kwa ushauri mwanamke anatakikana spate vipimo ama amuone daktari kwa vipimo na ushauri zaidi. Kama itakuwa sio kwababu ya mimba basi mgonjwa anatakikana kutumia Dawa zifuatazo ilikufanya hedhi itoke kama kawaida. 1. Chukua mvuje na pilipili manga chemsha pomoja na anywe kikombe cha kahawa kutwa Mara tatu. 2. Chukua manemane ichemshe na mgonjwa anywe asubuhi kabla ya kula kitu kwa mda wa siku tatu. Kwa Dawa na ushauri wa magonjwa mengine wasiliana nami +254732917064.