Zifahamu Nutrients na madini muhimu kwa Nguvu za Kiume. Siku hizi wanaume wengi wamekumbwa na tatizo la ukosefu wa nguvu za kiume kwa maana ya kutokuwa na uwezo wa kusimamisha uume wakati wa kufanya mapenzi, kushindwa kuendelea kusimamisha hadi mwisho wa tendo na kushindwa kurudia tendo hadi kuwaridhisha wenzi wao. Kadhalika wengine wamekuwa na tatizo la mbegu zao za kiume kutokuwa na umbile bora (sperm abnormalities) linaloziwezesha kusafiri kwa kasi ya kutosha katika uke wa mwanamke (sperm motility). Aidha wengine shahawa zao zina mbegu kidogo (low sperm count). Mwanaume anapomwaga shahawa wakati wa kufanya mapenzi shahawa hizo hupaswa kuwa na mbegu za kiume kiasi cha milioni 50 kwa kila milimita moja ya shahawa. Endapo kiasi hicho kitapungua chini ya miioni 20 uwezo wa uzazi (fertility) wa mwanaume huwa na kasoro. Matatizo yote hayo yanatokana na wanaunaume wengi kutokula vyakula sahihi au ulaji wa vyakula hivyo kwa kiwango kidogo ikilinganishwa na mahitaji ya m...