Skip to main content

TATIZO LA NGUVU ZA KIUME.

Zifahamu Nutrients na madini muhimu kwa Nguvu za Kiume.

Siku hizi wanaume wengi
wamekumbwa na tatizo la ukosefu wa nguvu za kiume kwa maana ya
kutokuwa na uwezo wa kusimamisha uume wakati wa kufanya mapenzi,

kushindwa kuendelea kusimamisha
hadi mwisho wa tendo na kushindwa kurudia tendo hadi kuwaridhisha wenzi wao.

Kadhalika wengine wamekuwa na tatizo la mbegu zao za kiume kutokuwa na umbile bora
(sperm abnormalities) linaloziwezesha kusafiri kwa kasi ya kutosha katika uke wa mwanamke (sperm motility).

Aidha wengine shahawa zao zina
mbegu kidogo (low sperm count).

Mwanaume anapomwaga shahawa
wakati wa kufanya mapenzi shahawa hizo hupaswa kuwa na mbegu za kiume kiasi cha milioni 50 kwa kila milimita moja ya shahawa.

Endapo kiasi hicho kitapungua chini ya miioni 20 uwezo wa uzazi (fertility) wa mwanaume huwa na kasoro.

Matatizo yote hayo yanatokana na
wanaunaume wengi kutokula vyakula sahihi au ulaji wa vyakula hivyo kwa kiwango kidogo ikilinganishwa na mahitaji ya mwili (Recommended Daily intake).

Tunaweza kupima ukweli kwamba
matatizo hayo yapo kwa kiwango
kikubwa kwa wingi wa matangazo ya madaktari na waganga wa tiba za
asili au tiba mbadala yanayotolewa
kwenye magazeti na mabango katika vituo vya magari au daladala na njia mbalimbali katika maeneo ya mijini.

Swali la kujiuliza mababu zetu mbona hawakuwa na matatizo haya?

Mbona walioa wake wengi na walimudu kuwatimizia haja zao za kimapenzi na walizaa watoto wengi?

Nini kimesababisha jamii yetu imekumbwa na matatizo hayo?

Jibu la maswali hayo ni rahisi sana! Tumeondoka kwenye mfumo wa asili wa ulaji vyakula vya asili na tumeingia kwenye mfumo wa ulaji vyakula visivyo vya asili au vilivyoondolewa uasili wake.

Sasa tuangalie viinilishe (nutrients) na madini yanayohitajika katika mwili wa mwanaume ili mwanaume huyo awe lijali na mwenye nguvu za kiume za kutosha.

1.Antioxidant Nutrients.

Upungufu wa vitamin E,vitamin C na selenium huwa na athari kwenye uzalishaji na uogeleaji wa shahawa
(sperm motility).

Tafiti zimeweza kuonyesha kwamba vitamin E kiasi cha vipimo vya kimataifa
(International Units - IU)100-200 kwa siku huboresha afya ya shahawa za mwanume asiyeweza
kumzalisha mwanamke
(infertile man) na kumwongezea uwezekano wa kumtia mimba
mwanamke.

Kadhalika vitamin C huongeza wingi wa mbegu za kiume kwenye
shahawa (sperm count)na uwezo wa shahawa kuogelea ndani ya uke wa mwanamke (sperm motility).

Tafiti pia zimeonyesha kwamba
selenium husaidia uogeleaji
wa shahawa. Mahitaji (Recommended Dietary Allowances – RDA)ya vitamin C ni miligramu 90.
Mwanaume anayevuta sigara
anahitaji miligramu 125.

Vyakula vyenye vitamin C ni pamoja na matunda jamii ya machungwa (citrus fruits),cantaloupe, kiwi, maembe,strawberries, broccoli,
cauliflower, pilipili nyekundu
na juisi ya nyanya.

Vitamin E RDA ni 15 IU (natural source)na 22 (synthetic).

Vyakula muhimu ni pamoja na ngano,karanga na jamii zake,
mafuta ya mimea, mbegu
zisizokobolewa (whole grains).

Selenium RDA ni 15 micrograms.

Vyakula muhimu vyenye selenium ni pamoja na samaki, seafood,
kuku, organ meats, whole grains, karanga na jamii zake (nuts), vitunguu, uyoga,vitunguu swaumu.


2.Vitamin B12.

Upungufu wa vitamin B12
hupelekea lower sperm counts na impaired sperm motility.

Vyakula muhimu vyenye B12 ni pamoja na nyama, kuku, samaki,
maziwa na bidhaa zake,mayai, soya na maziwa ya mchele (rice milk).


3.Zinc.

Madini ya zinc ni muhimu sana kwa masuala ya uzazi na uzalishaji wa shahawa.

Wanaume wenye matatizo ya uzazi wana upungufu wa madini ya zinc.

Upungufu wa madini hayo pia hupelekea wanaume kuwa na kiasi
kidogo cha homoni za kiume
(low testosterone levels).

Wanaume wenye shida hiyo
wakipewa madini ya zinc huwa na ongezeko la mbegu za kiume (increased sperm counts) na uwezo wa kutia mimba.RDA ya zinc ni
miligramu 11 kwa siku (wanawake huitaji miligramu 8).

Vyakula muhimu ni pamoja na pweza na chaza,dark turkey meat, lentils,ricotta cheese, tofu, yogurt,
spinach, broccoli, green beans, na juisi ya nyanya.

Hakikisha kwamba pamoja na madini ya zinc pia unapata madini ya copper kiasi cha miligramu moja
kwa siku kwa kuwa madini hayo hufanya kazi kwa pamoja kwa kutegemeana.

4.L-carnitine.

Husaidia kuongeza sperm count.

Utafiti mmoja uliofanywa ulibainisha kwamba gramu 3 kwa siku za L-carnitine kila siku kwa
muda wa miezi mitatu uli-saidia kuongeza sperm count na sperm motility kwa wanaume 37 kati ya 47. L-carnitine hupatikana kwenye
nyama na maziwa.

Kwa tiba kamili ya matatizo haya usisite kuwasiliana nami kwa +25732917064

Popular posts from this blog

TIBA YA ASILI YA FANGASI UKENI.

Fangasi ukeni ni muwasho sehemu ya ndani ya uke ambao unaweza kuambatana pia na kuvimba kwa uke. Leo sitaongelea sana juu ya nini kinasababisha hizi fangasi sehemu ya uke bali tutaona dozi kamili ya asili inayoweza kutibu kabisa tatizo hili linalosumbuwa wanawake wengi miaka sasa. Tumia dawa hizi 3 zote kwa pamoja ili kupata matokeo mazuri na usiache kuleta mrejesho hapa namna unavyoendelea: 1. LEMONADE Lemonade inaandaliwa kwa kutumia limau, maji, asali na mdalasini ya unga kidogo, nayo inaandaliwa hivi: *Chukua asali mbichi nusu Lita *Chukua limau kubwa 12 au zaidi, zikate katikati kila moja. Zikamuwe moja baada ya nyingine kupata maji maji ya limau mpaka umepata ujazo wa nusu lita. *Kwenye sufuria nyingine kubwa changanya mdalasini ya unga vijiko vikubwa 10 na maji lita 2 na nusu na uchemshe kama chai kisha ipua na uchuje na usubiri ipowe iwe ya uvuguvugu kidogo. *Sasa changanya pamoja asali nusu lita, juisi au maji maji ya limau nusu lita, maji ya uvuguvugu ya m...

TIBA YA MTU ALIEINGIWA NA JINNI SUGU.

kabla sijatoa tiba yake, ni lazima ujue unatibu nini na kwanini ni jinni. Maana zipo dalili mbalimbali zinazoonyesha mgonjwa amehusudiwa na jini na ni jini aina gani aliemuingilia muhusika. Zifuatazo ni aina na utaratibu wa kumtibu jini sugu. Dawa za kula. Habbatsaudai Habbatsufa Bakahadi Manimani Uzile Habbat rehani Karkam Halilinji Alhamza Kamun aswad Zamda Khardal Daarfilfil Filfil aswad Haltit Zaatar Harmal Sufa nyeupe Manimani Shomari Udinadi Ulinjani Sakabanji Kamun abyadh Uwatu Giligilani Karafuu Tangawizi Mdalasini Maua waridi Hakikisha dawa hizi umezitwanga na kuwa laini kisha utachukua kijiko kimoja cha kila dawa na kuchanganya kwenye asali safi ya nyuki lita moja na uisomee ruqya na mgonjwa awe anakunywa vijiko viwili mara tatu kwa siku kwa mda wa siku 30. NB Hakikisha wakati mgonjwa anatumia dawa za kula ambatanishe na za kujifukiza pamoja na za kujipaka. DAWA ZA KUFUKIZA kiribiti upele Sandarusi Haltit Karafuu maiti Mruturutu ...

KICHOMI

  Kichomi   ni moja ya dalili za ugonjwa moyo. Kupatwa kichomi mara moja moja si vibaya. Ukipatwa muda mrefu au kila wakati ; basi, chunguza zaidi. Kichomi husababishwa au kinaweza kuwa. Dalili ya matatizo ya tumbo lenye asidi (acid) kuzidi Dalili za ugonjwa wa moyo uitwao Ischemic Jambo la kuangalia ni je? Unashikwa kichomi ukiwa unatembea? Umeinama au umelala Ukishakula chakula Kama unapatwa kichomi wakati ukitembea au ukishafanya mazoezi makali ina maana kuna tatizo la damu kuingia sawasawa au kuzunguka (circulation) katika moyo. Kama unapatwa kichomi baada ya kula ina maana kuna tatizo katika chakula unachokula. Je mlo wako una acid(uchachu) sana? Je, unakula vyakula vyenye pilipili na binzari(spices) kwa wingi sana? Kama una kula sana vyakula vyenye asidi ina maana tumbo lako halimeng’enyui sawasawa linachoka. Kawaida binadamu unabidi kubadili badili ulaji. Usirudie vitu fulani fulani kila siku. Mathalan usiweke pilipili katika kila mlo. Tatizo ji...