Akina mama wengi huwa wanapata matatizo ya kuvimba miguu wakati wa ujauzito kwa sababu mbalimbali. Wengine huwa ni kawaida kwa maana ya kwamba haisababishwi na ugonjwa wa aina yoyote. Wakati mimba inapokua kubwa huweza tumbo la uzazi Uterus hukandamiza mishipa ya damu inayorudisha damu kwenye moyo Veins au ile mishipa inayobeba maji damu lymph kutoka kwenye miguu. Hali hiyo hufanya damu na hayo maji damu kushindwa kurudi yote kwenye moyo na kujikusanya sehemu ambazo ni Dependent hasa miguuni na kusababisha uvimbaji wa miguu Dependent Oedema. Uvimbaji huu ni ule ambao sana uko kwenye sehemu ya mguu chini ya kifundo cha mguu Ankle Oedema, kama miguu ikivimba kupanda juu hadi kwenye mapaja au juu zaidi hii huwa ni dalili ya ugonjwa. Magonjwa ambayo yanaweza kusababisha uvimbe miguuni na sehemu nyingine za mwili wa mjamzito ni pamoja na kuwa na shinikizo la damu la ujauzito Pre-eclampsia, magonjwa ya figo ambapo mtu huvimba miguu, uso pia, magojwa ya ini – haya husababisha p...