Skip to main content

Posts

Showing posts from September 6, 2017

KICHOMI

  Kichomi   ni moja ya dalili za ugonjwa moyo. Kupatwa kichomi mara moja moja si vibaya. Ukipatwa muda mrefu au kila wakati ; basi, chunguza zaidi. Kichomi husababishwa au kinaweza kuwa. Dalili ya matatizo ya tumbo lenye asidi (acid) kuzidi Dalili za ugonjwa wa moyo uitwao Ischemic Jambo la kuangalia ni je? Unashikwa kichomi ukiwa unatembea? Umeinama au umelala Ukishakula chakula Kama unapatwa kichomi wakati ukitembea au ukishafanya mazoezi makali ina maana kuna tatizo la damu kuingia sawasawa au kuzunguka (circulation) katika moyo. Kama unapatwa kichomi baada ya kula ina maana kuna tatizo katika chakula unachokula. Je mlo wako una acid(uchachu) sana? Je, unakula vyakula vyenye pilipili na binzari(spices) kwa wingi sana? Kama una kula sana vyakula vyenye asidi ina maana tumbo lako halimeng’enyui sawasawa linachoka. Kawaida binadamu unabidi kubadili badili ulaji. Usirudie vitu fulani fulani kila siku. Mathalan usiweke pilipili katika kila mlo. Tatizo ji...

FIBROID

Fibroid ni uvimbe ambao hutokea kwenye tumbo la kizazi ambao huu uvimbe unaweza kuwa ndani ya kizazi(ukutani mwa kizazi) au ndani ya nyama ya kizazi na nje kwenye ukuta wa kizazi. Kuna aina kuuzifuatazo za fibroids:  1.Submucosal fibroids(ndani ya kizazi)  2.Intramural fibroid(ndani ya nyama za kizazi)  3. Subserosal(nje ya kizazi).  Watu wafuatao wako hatarini ya kupata ugonjwa huu fibroids  1.Mwanamke ambae hajawahi kupata mtoto mpaka umri mkubwa  2.Miaka kuanzia kubarehe mpaka hedhi kukoma  3.Kurithi  4.Unene  5.Kuingia hedhi mapema Fibroids sio kansa ni uvimbe wa kawaida tu ambao unakua kwa kutegemea kichocheo cha estrogen hormone ndio maana kuanzia kubarehe mpaka kukoma kwa hedhi ndio wako hatarini. Na mara nyingi uvimbe huu waga unaongezeka kukua sana hasa wakati wa ujauzito kwani vichocheo hivi huongezeka wakati huu kulinda makazi ya mtoto. Ni watu waliofikia kikomo cha hedhi hawapati fibroids au kitaalam leomyoma....

UTATIZO LA UGUMBA KWA WANAWAKE

Ugumba kwa mwanamke ni tatizo la mwanamke kushindwa kushika mimba licha ya kushiriki kufanya mapenzi na mwanamume bila kutumia kinga. Tatizo la kutoshika mimba kwa kipindi angalau mwaka mmoja huku mwanamke huyo akishiriki kikamilifu ufanyaji mapenzi na mwanamume huitwa ugumba (Sterility). Ugumba kwa mwanamke (Sterility) sio sawa au haina maana sawa na tatizo la mwanamke kutojisikia au kutokuwa na hisia za kufanya mapenzi yaani ‘Frigidity’. Zipo sababu nyingi zinazoweza kufanya mwanamke awe mgumba. Mwanamume pia anaweza kuwa chanzo cha ugumba kwa maana kwamba hana uwezo wa kutungisha mimba. Hivyo,ndio kusema mwanaume kamwe hapaswi kumlaumu mwanamke anayeshirikiana naye kimapenzi kuwa ndiye ‘mgumba’ wakati mwanamume na mwanamke kwa pamoja wana asilimia sawa za kuwa chanzo cha ugumba. Ndio maana mwanamume na mwanamke wanapooana na wakashiriki ngono kikamilifu kwa kipindi cha mwaka mmoja, lakini hakuna dalili za mwanamke kuwa mjamzito, basi wote wawili wanapas...