Skip to main content

FIBROID

Fibroid ni uvimbe ambao hutokea kwenye tumbo la kizazi ambao huu uvimbe unaweza kuwa ndani ya kizazi(ukutani mwa kizazi) au ndani ya nyama ya kizazi na nje kwenye ukuta wa kizazi.

Kuna aina kuuzifuatazo za fibroids: 

1.Submucosal fibroids(ndani ya kizazi) 

2.Intramural fibroid(ndani ya nyama za kizazi) 

3. Subserosal(nje ya kizazi).


 Watu wafuatao wako hatarini ya kupata ugonjwa huu fibroids 
1.Mwanamke ambae hajawahi kupata mtoto mpaka umri mkubwa 

2.Miaka kuanzia kubarehe mpaka hedhi kukoma 

3.Kurithi 

4.Unene 

5.Kuingia hedhi mapema Fibroids sio kansa ni uvimbe wa kawaida tu ambao unakua kwa kutegemea kichocheo cha estrogen hormone ndio maana kuanzia kubarehe mpaka kukoma kwa hedhi ndio wako hatarini. Na mara nyingi uvimbe huu waga unaongezeka kukua sana hasa wakati wa ujauzito kwani vichocheo hivi huongezeka wakati huu kulinda makazi ya mtoto. Ni watu waliofikia kikomo cha hedhi hawapati fibroids au kitaalam leomyoma. 


Dalili za fibroids 
1.Kutokwa damu kwenye via vya uzazi katikati ya mwezi. 

2.Kutokwa na uchafu wenye harufu mbaya au ambao hauna harufu lakini mwingi na mweupe. 

3.Maumivu ya kiuno hasa wakati wa hedhi ambayo husababishwa na kizazi kujaribu kusukuma huo uvimbe.wengi hupata maumivu makali sana. 

4.Tumbo kuuma sana chini ya kitovu. 

5.Hedhi zisizokuwa na mpango 

6.Maumivu wakati wa tendo la ndoa 

7.Kukosa hamu ya tendo la ndoa 

8.Maumivu makali wakati wa hedhi Uvimbe.



 unapokua mkubwa unaweza kusababisha dalili zifuatazo;

1.Kukojoa mara kwa mara kwani uvimbe unakandamiza kibofu cha mkojo 

2.Mkojo kubaki kwenye kibofu cha mkojo 

3.Haja kuwa ngumu 

4.Miguu kuvimba 

5.Kupungukiwa damu. 



Jinsi fibroids zinavyoweza kuzuia kupata mtoto: 

1.Fibriods zikikua sana zinakandamiza mishipa ya kupitisha mayai kutoka kwenye kiwanda yan ovari 

2.Uvimbe pia unazuia yai lililorutubishwa kujishikiza kwenye kizazi..hasa submucosal fibroids 

3.Pia husuia mfuko wa kizazi kukaza kusukuma mbegu kwenda kwenye mishipa ya kupitisha mayai. 

Comments

Popular posts from this blog

TIBA YA MTU ALIEINGIWA NA JINNI SUGU.

kabla sijatoa tiba yake, ni lazima ujue unatibu nini na kwanini ni jinni. Maana zipo dalili mbalimbali zinazoonyesha mgonjwa amehusudiwa na jini na ni jini aina gani aliemuingilia muhusika. Zifuatazo ni aina na utaratibu wa kumtibu jini sugu. Dawa za kula. Habbatsaudai Habbatsufa Bakahadi Manimani Uzile Habbat rehani Karkam Halilinji Alhamza Kamun aswad Zamda Khardal Daarfilfil Filfil aswad Haltit Zaatar Harmal Sufa nyeupe Manimani Shomari Udinadi Ulinjani Sakabanji Kamun abyadh Uwatu Giligilani Karafuu Tangawizi Mdalasini Maua waridi Hakikisha dawa hizi umezitwanga na kuwa laini kisha utachukua kijiko kimoja cha kila dawa na kuchanganya kwenye asali safi ya nyuki lita moja na uisomee ruqya na mgonjwa awe anakunywa vijiko viwili mara tatu kwa siku kwa mda wa siku 30. NB Hakikisha wakati mgonjwa anatumia dawa za kula ambatanishe na za kujifukiza pamoja na za kujipaka. DAWA ZA KUFUKIZA kiribiti upele Sandarusi Haltit Karafuu maiti Mruturutu ...

KUONDOSHA MARADHI YA SUBIAN NA KUONDOA WASIWASI

Kwa mtu mwenye matatizo hayo achukue dawa zifuatazo :- - unga wa ambari nyeusi. - unga wa mvuje. - unga wa kitunguu thaum. - mafuta ya uto. - mafuta original ya zaituni. Maelezo Changanya na iwe unajipaka mwili mzima asubuhi na jioni kwa mda wa siku 21.

UTOSI KUINGIA NDANI KWA MTOTO MCHANGA.

chukua manjano mbichi iponde iwe laini sana, kisha chukua pamba na uiweke ile dawa, kisha muekee mtoto mchanga aliena tatizo hilo utosini. In shaa allah utosi utarudi sawa. Utafanya hivyo kwa siku mara moja mpaka tatizo litakapokwisha.