Skip to main content

UTATIZO LA UGUMBA KWA WANAWAKE

Ugumba kwa mwanamke ni tatizo la
mwanamke kushindwa kushika mimba licha ya kushiriki kufanya mapenzi na mwanamume bila kutumia kinga.


Tatizo la kutoshika mimba kwa kipindi angalau mwaka mmoja huku mwanamke huyo akishiriki kikamilifu ufanyaji mapenzi na mwanamume huitwa ugumba (Sterility).


Ugumba kwa mwanamke (Sterility) sio sawa au haina maana sawa na tatizo la mwanamke kutojisikia au kutokuwa na hisia za kufanya mapenzi yaani ‘Frigidity’.



Zipo sababu nyingi zinazoweza kufanya mwanamke awe mgumba.


Mwanamume pia anaweza kuwa chanzo cha ugumba kwa maana kwamba hana uwezo wa kutungisha mimba.


Hivyo,ndio kusema mwanaume kamwe hapaswi kumlaumu mwanamke anayeshirikiana naye kimapenzi kuwa ndiye ‘mgumba’


wakati mwanamume na mwanamke kwa pamoja wana asilimia sawa za kuwa chanzo cha ugumba.


Ndio maana mwanamume na mwanamke wanapooana na wakashiriki ngono kikamilifu kwa kipindi cha mwaka mmoja,

lakini hakuna dalili za mwanamke kuwa mjamzito,


basi wote wawili wanapaswa kwenda kwa pamoja kwa watalaamu wa masuala ya afya ya uzazi ili kuchunguzwa kwa kufanyiwa vipimo.


Ili mwanamke apate ujauzito
mwanamume hukojoa shahawa
kwenye uke wa mwanamke.


Shahawa husafiri kwenye uke wa mwanamke kupitia mirija ya uzazi(fallopian tube)kwenda kurutubisha yai la mwanamke(ova).


Sasa ili mbegu za kiume (sperms) ziwe salama wakati zinasafiri katika uke wa mwanamke lazima majimaji katika uke yawe katika hali ya nyongo(alkaline fluid).


Kama majimaji ya uke yakiwa hayako katika hali ya nyongo yaani ni tindikali(acid)mbegu za kiume zitakufa na hakutokuwa na uwezo wa urutubishwaji wa yai la mwanamke.


Ili majimaji ya uke wa mwanamke yawe katika hali inayotakiwa ya alkaline kuna mambo mawili ni muhimu sana.


Moja,

👉mishipa ya neva katika uke wa mwnamke iwe inafanya kazi zake sawasawa.


Mwanamke mwenye mawazo sana (nervous)sio rahisi kupata ujauzito.


Hivyo ili neva ifanye kazi sawasawa mwanamke hapaswi kuwa mtu mwenye mawazo au mwenye kuudhiwa,

anapaswa kula milo kamili na anapaswa kuwa na muda wa
kupumzisha akili yake(adequate rest
and relaxation).


Jambo la pili,


👉mwanamke anapaswa kula vyakula vinavyotengeneza alkali katika mwili ambavyo ni mboga za majani na matunda,pia kuepuka kula kwa wingi vyakula vinavyoleta asidi katika mwili.


Sasa tuangalie visababishi vya tatizo la ugumba kwa mwanamke.


Visababishi hivyo ni pamoja na mapungufu ya viungo vya uzazi vya mwanamke(physicaldefects or structural abnormalities of genitals
and reproductive organs).


Mwanamke anaweza kuwa ama
amezaliwa na mapungufu hayo katika mji wa mimba (womb) au njia ya uzazi (fallopian tubes) au aliyapata kutokana na ajari.



Sababu nyingine huitwa ‘Physical debility’

yaani mwanamke kutokuwa na afya bora ya mwili kutokana na magonjwa yaliyompata na yakadumu katika mwili wake wa kipindi kirefu(magonjwa sugu).


Magonjwa hayo ni pamoja na magonjwa ya zinaa.

Kadhalika upungufu wa damu
(Anaemia),

kukosa choo ipasavyo
(constipation)

au mwanamke kuwa na uzito mkubwa(obesity)

au uzito mdogo ambao hautakiwi kitalaamu yaani kwa vipimo vya Body Mass Index (BMI).


huweza kufanya mwanamke asipate ujauzito.



Visababishi vingine ni mwili wa mwanamke kutokuzalisha homoni muhimu za uzazi na kutokupata mzunguko mzuri wa hedhi (lack of normal menstrual cycle)


sanjari na matatizo ya kisaikolojia hususan mwanamke anapoudhiwa au anapokuwa na mawazo kutokana na kutokuzaa mtoto mapema (emotional stress,tension,mental depression,anxiety,and fear).



Matibabu kwa visababishi aina ya
‘physical defects’

mwanamke anapaswa kwenda kufanyiwa vipimo na watalaamu wa masuala ya afya ya uzazi na kushauriwa ipasavyo mambo ya kufanya.



Matibabu kwa visababishi aina ya ‘physical debility’

huweza kutibika kwa njia za kawaida tu kwa kula vyakula vinavyotakiwa,

kujijali na kuuheshimu mwili(yaani usafi na kujikinga na maambukizi)
na kufuata sheria za asili(laws of
nature).


Mwanamke mwenye tatizo la
ugumba ambalo sio la mapungufu katika viungo vya uzazi anashauriwa kuanza matibabu kwa njia ya asili.


Kwanza aanze kwa kufunga bila kula
kwa siku mbili huku akitumia maji ya kutosha kwa ajili ya kusafisha taka katika mwili.


Baada ya hapo ale mlo kamili ambao takriban asilimia 70-80 ya vyakula viwe havikupikwa(in their natural uncooked states)

kwa sababu upikaji wa vyakula
hupunguza au huaribu viinilishe (nutrients)vilivyomo kwenye vyakula.


Mlo uwe na vyakula vya mbegu (seeds,nuts and grains),mboga za majani na matunda.


Katika milo hiyo tumia pia maziwa na asali.


Mafuta unayotumia katika vyakula
yawe yale ya mimea(vegetable oils).


Ili mwanamke awe na mwili wenye afya njema nashauri afuate ratiba hii ya milo.



Asubuhi akiamka,

anywe glasi moja ya maji vuguvugu yaliyotiwa limao.


Kifungua kinywa(breakfast) ijumuishe matunda(fresh fruits) kama apples,chungwa,ndizi,zabibu, na balungi na maziwa glasi moja.



Chakula cha mchana.


ale mboga za majani zilizochemshwa kiasi(zisiive kabisa) na ziungwe kwa mafuta ya mimea au siagi na chumvi kiasi,chapatti mbili au tatu na maziwa(a glass of buttermilk).


Katika kipindi cha kati ya mlo wa mchana (lunch) na mlo wa jioni/usiku (dinner).


anywe juisi ya matunda(fresh)au juisi ya mboga za majani.


Chakula cha usiku,


ale saladi nyingi inayotokana na mboga za majani(fresh vegetables) kama nyanya,karoti,viazi sukari (beetroots),na vitunguu na
maharage au jamii ya maharage yalipikwa.



Wakati wa kwenda kulala,


ale apple au maziwa glasi moja.


Mwanamke aepuke kula vyakula vyenye mafuta mengi,viungo vikali,
chai iliyokolea sana majani,kahawa,
sukari nyeupe(white sugar)na unga
mweupe uliokobolewa (white flour).
Unywaji wa pombe na uvutaji sigara
viepukwe.



Matibabu mengine ambayo husaidia
kutibu tatizo la ugumba kwa mwanamke ni kutumuia mzizi wa mti uitwao ‘banyan’.


Chukua mzizi huo na ukaushe sio kwa kuuweka juani bali kivulini mpaka ukauke.


Baada ya hapo unausaga kuwa unga.

Changanya unga huo na maziwa na tumia usiku wakati wa kwenda kulala kwa siku tatu.


Usitumie pamoja na chakula au kinywaji chochote wakati wa usiku.


Namna ya kuchanganya:

pima kwa uzito,unga wa banyani uwe na uzito mara tano ya uzito wa
maziwa.



Tiba nyingine ni mwanamke kula bilinganya(eggplants)zilizopikwa.


Ale pamoja na maziwa buttermilk kila siku kwa mwezi mmoja au miezi miwili hivi.


Mlo huu huongeza mwilini homoni ya uzazi iitwayo progesterone na pia huongeza uwezo wa mwili kutumia vitamin E inayopatikana kwenye chakula anachokula.


Bila kusahau mwanamke ahakikishe anakuwa na uwiano wa uzito na urefu wa mwili unaostahili.


Kwa upande wa dawa zilizoandaliwa kitaalamu anaweza kuwasiliana na
+254732917064

Comments

Popular posts from this blog

TIBA YA ASILI YA FANGASI UKENI.

Fangasi ukeni ni muwasho sehemu ya ndani ya uke ambao unaweza kuambatana pia na kuvimba kwa uke. Leo sitaongelea sana juu ya nini kinasababisha hizi fangasi sehemu ya uke bali tutaona dozi kamili ya asili inayoweza kutibu kabisa tatizo hili linalosumbuwa wanawake wengi miaka sasa. Tumia dawa hizi 3 zote kwa pamoja ili kupata matokeo mazuri na usiache kuleta mrejesho hapa namna unavyoendelea: 1. LEMONADE Lemonade inaandaliwa kwa kutumia limau, maji, asali na mdalasini ya unga kidogo, nayo inaandaliwa hivi: *Chukua asali mbichi nusu Lita *Chukua limau kubwa 12 au zaidi, zikate katikati kila moja. Zikamuwe moja baada ya nyingine kupata maji maji ya limau mpaka umepata ujazo wa nusu lita. *Kwenye sufuria nyingine kubwa changanya mdalasini ya unga vijiko vikubwa 10 na maji lita 2 na nusu na uchemshe kama chai kisha ipua na uchuje na usubiri ipowe iwe ya uvuguvugu kidogo. *Sasa changanya pamoja asali nusu lita, juisi au maji maji ya limau nusu lita, maji ya uvuguvugu ya m...

TIBA YA MTU ALIEINGIWA NA JINNI SUGU.

kabla sijatoa tiba yake, ni lazima ujue unatibu nini na kwanini ni jinni. Maana zipo dalili mbalimbali zinazoonyesha mgonjwa amehusudiwa na jini na ni jini aina gani aliemuingilia muhusika. Zifuatazo ni aina na utaratibu wa kumtibu jini sugu. Dawa za kula. Habbatsaudai Habbatsufa Bakahadi Manimani Uzile Habbat rehani Karkam Halilinji Alhamza Kamun aswad Zamda Khardal Daarfilfil Filfil aswad Haltit Zaatar Harmal Sufa nyeupe Manimani Shomari Udinadi Ulinjani Sakabanji Kamun abyadh Uwatu Giligilani Karafuu Tangawizi Mdalasini Maua waridi Hakikisha dawa hizi umezitwanga na kuwa laini kisha utachukua kijiko kimoja cha kila dawa na kuchanganya kwenye asali safi ya nyuki lita moja na uisomee ruqya na mgonjwa awe anakunywa vijiko viwili mara tatu kwa siku kwa mda wa siku 30. NB Hakikisha wakati mgonjwa anatumia dawa za kula ambatanishe na za kujifukiza pamoja na za kujipaka. DAWA ZA KUFUKIZA kiribiti upele Sandarusi Haltit Karafuu maiti Mruturutu ...

KICHOMI

  Kichomi   ni moja ya dalili za ugonjwa moyo. Kupatwa kichomi mara moja moja si vibaya. Ukipatwa muda mrefu au kila wakati ; basi, chunguza zaidi. Kichomi husababishwa au kinaweza kuwa. Dalili ya matatizo ya tumbo lenye asidi (acid) kuzidi Dalili za ugonjwa wa moyo uitwao Ischemic Jambo la kuangalia ni je? Unashikwa kichomi ukiwa unatembea? Umeinama au umelala Ukishakula chakula Kama unapatwa kichomi wakati ukitembea au ukishafanya mazoezi makali ina maana kuna tatizo la damu kuingia sawasawa au kuzunguka (circulation) katika moyo. Kama unapatwa kichomi baada ya kula ina maana kuna tatizo katika chakula unachokula. Je mlo wako una acid(uchachu) sana? Je, unakula vyakula vyenye pilipili na binzari(spices) kwa wingi sana? Kama una kula sana vyakula vyenye asidi ina maana tumbo lako halimeng’enyui sawasawa linachoka. Kawaida binadamu unabidi kubadili badili ulaji. Usirudie vitu fulani fulani kila siku. Mathalan usiweke pilipili katika kila mlo. Tatizo ji...