Skip to main content

UGONJWA WA STROKE ( KIHARUSI )

UGONJWA WA STROKE(KIHARUSI)
Fahamu aina za kiharusi(strocke).


Kiharusi au kwa Kiingereza Stroke ni kitendo cha baadhi ya viungo vya mwili kuwa na ganzi au kutojiweza kufanya kazi zake za kawaida.


Kuna aina mbili za kiharusi,


lakini kabla ya kuchambua hayo tuangalie,ni nini kinasababisha mtu
kukumbwa na ugonjwa huu ?.


Mtu anaweza kupata dalili za ugonjwa huu wa kiharusi na baada ya dakika chake zikaisha.


Kiharusi kinampata binadamu baada ya eneo la ubongo kukosa damu kwa saa 24 ama zaidi au kunapotokea kizuizi cha damu au mishipa ya damu kushindwa kusafirisha damu au mshipa huo
unapopasuka.


Kiharusi kimegawanyika katika aina kuu mbili kulingana na jinsi kinavyotokea.


kwanza ni:

1.Kiharusi cha kukosa hewa kwenye ubongo kitaalamu huitwa Ischemic stroke.

(Ischemic ni neno la Kigiriki lenye maana ya kuzuia damu).


Aina hii ya kiharusi hutokea iwapo usambazaji wa damu katika sehemu ya ubongo hupungua na kusababisha tishu za ubongo za eneo lililoathirika kushindwa kufanya kazi zake vizuri.


Hiki hutokea baada ya mshipa wa ateri kuziba kutokana na kuganda kwa damu,hali ambayo inasababisha damu isisafiri vyema na kuelekea kwenye ubongo.


Hali hiyo pia hufanya damu iliyoganda kuziba mishipa midogo ndani ya ubongo kitaalamu huitwa Cerebral thrombosis au kipande cha damu kumeguka na kwenda kuziba mshipa wa damu kwenye ubongo kitaalamu huitwa Cerebral embolism.


Lakini tatizo hili linaweza kutokea pale damu inapoganda sehemu nyingine ya mwili na kusafiri hadi kwenye mishipa ya ateri,hivyo kusababisha damu kwenda kwenye ubongo kukwama.


Hata hivyo,tatizo hili linaweza
kusababisha kitu kinachoitwa Lacunar stroke,yaani vimirija vidogovidogo sana vya damu vilivyopo ndani ya ubongo,vinaziba.


Hapo sasa binadamu huwa anakumbwa na kiharusi kinachojulikana kitaalamu Lacunar stroke japokuwa mara nyingi hii haiwaletei sana shida wagonjwa.


KIHARUSI CHA HAEMORRHAGE.

Baada ya kufafanua kiharusi kinachoitwa ischaemia ambacho ndani yake tukaelezea pia kile kinachoitwa Lacunar stroke,sasa tuelezee aina ya kiharusi kiitwacho Haemorrhage.


Aina hii ya kiharusi,mrija wa damu karibu ama kwenye ubongo hupata mpasuko hivyo kusababisha damu kuvuja na kitendo hicho ndicho kitaalamu huitwa Haemorrhage.


Kinachotokea ni kwamba damu inayovuja hukandamiza ubongo na kuuharibu,ubongo ni moja ya kiungo laini sana mwilini.Katika hali ya kitaalamu inayoitwa Intra cerebral haemorrhage,uvujaji wa damu hufanyika ndani ya ubongo wenyewe.


Mara nyingi aina hii ya kiharusi hutanguliwa na dalili za kichwa kuuma,au kuwepo kwa historia ya ajali ya kichwa.



Lakini kuna hali pia inayoitwa Subarachnoid haemorrhage ambapo mpasuko wa mshipa wa damu hufanyika karibu na eneo linalozunguka ubongo linaloitwa Subarachnoid.



Wakati fulani,mishipa ya damu huzungukwa na aina fulani za mafuta yasiyofaa mwilini,hali inayoitwa kitaalamu kama Atherosclerotic plaque.


Hali hii husababisha kuganda kwa damu katika mishipa (thrombosis) hiyo.

DALILI ZA STROKES AU KIHARUSI
- kuchanganyikiwa,mtu kupata shida ya kuongea na kuelewa anachoambiwa.
- Maumivu ya kichwa pamoja na kupoteza fahamu kwa vipindi na kutapika
- Ganzi usoni,mkono na mguu na hasa ikiwa ni stroke ya upande mmoja wa mwili
- shida ya kuona
- Shida ya kutembea
Kizunguzungu na kukosa mpangilio wa matendo ya mwili

BAADHI YA ATHARI
- maumivu ya mikono na miguu baada ya viungo hvyo kufanya kazi au kutokea mabadiliko ya hali ya hewa
- Msongo wa mawazo
- Kupooza au udhaifu wa upande1
- Kupata shida ktk kuonyesha hisia za mwili
- Kushindwa kumudu matumizi ya kibofu cha mkojo au viungo vya njia ya haja kubwa

JINSI YA KUZUIA STROKE
- Usitumie dawa za kulevya
- Kula chakula chenye mboga na matunda kwa wingi na chenye cholestrol kidogo.
- Fanya mazoez kila siku
- Hakikisha unadhibiti kiwango cha sukari mwilini
- Jitahidi kupunguza uzito
Acha pombe na sigara

tunazo dawa kamili za kuchua, kunywa za maradhi haya.
+254732917064

Popular posts from this blog

MDUDU WA KIDOLE

Huu ni ugonjwa unaoathiri vidole vya miguu na mikono, sana sana unaathiri mikononi nadra sana mguuni.tatizo hili lisipotibiwa kwa mapema linaweza hata kufanya kidole kikakatika. Zifuatazo ni tiba za kutibu maradhi Haya :-  Njia ya kwanza Chukua mbaazi kidogo kisha ziroweke kwenye maji kwa mda mpaka zilainike, halafu utaziweka kwenye kinu na kuzitwanga mpaka zilainike, ukikosa kinu tumia kitu chochote cha kusagia ili tu ziwelaini sana. Halafu utachukua dawa hiyo na kupaka kwenye sehemu iliyoathirika na kufunga kwa kitambaa usiku mzima. Na ukiamka itakuwa imechuja uchafu wote na kufanya sehemu iliyoathirika kupona, ikiwa bado toa hiyo dawa na kufunga nyengine. Kwa uwezo was ALLAH dawa hii utapona na no mujarrab. Njia ya pili Tiba hii ni kwa mdudu anaeanza sasa kabla hajaiva na kuwa rangi ya njano. Chukua kitunguu thaum kisage kiwe laini na upake sehemu iliyoathirika kwa mda was masaa 12 kisha toa na kupaka nyengine mpaka utakapo pata nafuu. Mpemba herbal +254732917064...

UTOSI KUINGIA NDANI KWA MTOTO MCHANGA.

chukua manjano mbichi iponde iwe laini sana, kisha chukua pamba na uiweke ile dawa, kisha muekee mtoto mchanga aliena tatizo hilo utosini. In shaa allah utosi utarudi sawa. Utafanya hivyo kwa siku mara moja mpaka tatizo litakapokwisha.

HEDHI KUTOKA KIDOGO KIDOGO.

hii Mara nyingi inasababishwa na mambo kadhaa ikiwemo hormone imbalance, kutumia Dawa za family planning na matatizo mbali mbali yanayompata mwanamke ndani ya mwezi uliopita. Kwa ushauri mwanamke anatakikana spate vipimo ama amuone daktari kwa vipimo na ushauri zaidi. Kama itakuwa sio kwababu ya mimba basi mgonjwa anatakikana kutumia Dawa zifuatazo ilikufanya hedhi itoke kama kawaida. 1. Chukua mvuje na pilipili manga chemsha pomoja na anywe kikombe cha kahawa kutwa Mara tatu. 2. Chukua manemane ichemshe na mgonjwa anywe asubuhi kabla ya kula kitu kwa mda wa siku tatu. Kwa Dawa na ushauri wa magonjwa mengine wasiliana nami +254732917064.