Skip to main content

MABUSHA

Kwa undani kuhusu mabusha.


Mabusha ni hali ya kujaa maji kwenye mfuko wa pumbu. Hali hii hutokea kunapokuwa na mkusanyiko wa maji kati ya tabaka mbili za utando unaozunguka korodani.



Dalili za Mabusha.

Katika hatua za awali, mabusha hayana dalili zozote (asymptomatic).

Hata hivyo, baada ya muda fulani,
mapumbu hujaa na uvimbe huweza
kuonekana hata kwa nje. Kwa kadiri
uvimbe unavyozidi kuongezeka, dalili zifuatazo zaweza kujitokeza pia;

Muhusika kujihisi hali ya uzito na
kuvuta sehemu za siri kutokana na
kujaa na kuongezeka kwa uzito wa
mapumbu.

Mgonjwa huweza kujihisi hali ya
usumbufu na kutojisikia vizuri maeneo ya kinena mpaka mgongoni.

Kwa kawaida mabusha hayana
maumivu yeyote. Hata hivyo, iwapo
mgonjwa ataanza kujihisi maumivu,
hiyo ni dalili ya kuwepo kwa uambukizi katika mshipa wa epididymis (acute epididymitis).

Uvimbe huwa na tabia ya kupungua
iwapo mgonjwa atakaa kitako na
huongezeka pindi anaposimama.

Iwapo mgonjwa atajisikia homa,
kichefuchefu na kutapika, hizo ni dalili za kuwepo kwa uambukizi katika mabusha.

Kwa kawaida mabusha hayana
muingiliano na uwezo na ufanisi wa
utendaji wa ngono. Hata hivyo kuna
taarifa tofauti za kitafiti kutoka bara
Asia na Afrika Magharibi kuwa mabusha yanaweza kuathiri ufanisi wa ngono na kwa kiasi fulani kusababisha mhemko au msongo wa mawazo kwa muathirika.



Mabusha husababishwa na nini?.

Sababu za kutokea kwa mabusha
hutofautiana kati ya watoto wa kiume na wanaume watu wazima.

Kwa watoto wa kiume Kwa watoto wa kiume, mabusha huweza kuanza kutokea kipindi cha ujauzito.

Wakati wa ujauzito, korodani za mtoto wa kiume huwa kwenye tumbo lake kabla ya kushuka taratibu kuelekea kwenye mapumbu. Wakati wa ushukaji huo, kifuko kinachozunguka korodani
kinachoitwa processus vaginalis
hushuka sambamba na kurodani hizo na kufanya korodani kuzungukwa na maji.

Kwa kawaida, ndani ya muda wa
mwaka mmoja, kifuko hiki hufunga na maji hayo yanayozunguka korodani yote hufyonzwa na kurudishwa kwenye tumbo la mtoto.Iwapo baada ya kifuko
kufunga na maji yaliyomo kushindwa kufyonzwa kurudishwa kwenye tumbo la mtoto, mtoto hupata busha lijulikanalo kitaalamu kama busha lisilo na mawasiliano (non-communicating hydrocele).

Hali kadhalika, wakati mwingine
inawezekana kifuko kikashindwa
kufunga na hivyo maji yakaendelea
kujaa ndani ya kifuko kuzunguka
korodani. Aina hii ya mabusha kwa
watoto ujulikana kama busha lenye
mawasiliano (communicating
hydrocele).

Kwa wanaume watu wazima Kwa wanaume watu wazima, mabusha husababishwa na mambo makuu mawili; Kwanza, kitendo chochote kinachochochea tando zinazozunguka korodani kuzalisha maji kwa wingi kuliko kawaida, na njia ya pili ni kupungua kwa ufyonzaji wa maji yanayozunguka korodani kwa sababu ya kuziba kwa mirija ya lymph (blockage of scrotal lymphatic system) au kuziba kwa mishipa ya damu inayosafirisha damu kutoka kwenye pumbu kwenda sehemu nyingine za mwili (blockage of scrotal venous system).

Ongezeko la uzalishaji wa maji linaweza kutokana na Maambukizi au/na majeraha katika korodani (testicular inflammation au
orchitis) au maambukizi katika mshipa ujulikanao kama epididymis yanayoweza kusababishwa na kifua kikuu (tuberculosis) cha makende, au maambukizi yanayosababishwa na vimelea wa filaria (filariasis)
wanaosababishwa na kuumwa na mbu aina ya Culex.

Kujinyonga kwa korodani (testicular
torsion) kunakoweza kuzifanya korodani kutenda kazi zaidi ya kiwango chake (hyperactive testis).

Uvimbe katika korodani (testicular
tumors) ambao husababisha uzalishaji wa maji kupita kiasi.

Kupungua kwa ufyonzaji wa maji
hutokana na ufanyiwa upasuaji kipindi cha siku za nyuma katika eneo la kinena, au operesheni ya upandikizaji figo ambazo zinaweza kuathiri mfumo wa lymph na vena na hivyo kupunguza ufyonzaji wa
maji kutoka kwenye mapumbu.

Kuwahi kufanyiwa tiba ya mionzi kipindi cha nyuma nayo uhusishwa na kutokea kwa mabusha.

Kwa hapa kwetu Tanzania, kung’atwa na mbu aina ya Culex anayeeneza vimelea vya filaria kunaelezwa kuwa sababu kuu mojawapo inayopelekea kuwepo kwa tatizo la mabusha na matende hususani maeneo ya Pwani na
mwambao.


Madhara ya Mabusha Kwa kawaida mabusha hayana madhara yeyote. Aidha mabusha hayawezi kuathiri uwezo wa mtu kuzaa.

Hata hivyo mabusha yanaweza kuleta madhara iwapo tu kama yakiambatana na magonjwa mengine kwenye korodani.

Kwa mfano, kama mabusha
yataambatana na maambukizi
(testicular infection) au uvimbe kwenye korodani (testicular tumor), yanaweza kusababisha kupungua kwa uzalishaji na utendaji kazi wa mbegu za kiume (sperms) na kupelekea tatizo la ugumba
kwa wanaume.

Hali kadhalika, iwapo sehemu ya
utumbo mkubwa au mdogo imebanwa katika upenyo fulani kwenye sehemu ya ukuta wa tumbo, huweza kusababisha ngiri (strangulated hernia), hali ambayo
ni hatari kama isipotibiwa haraka.

Popular posts from this blog

TIBA YA ASILI YA FANGASI UKENI.

Fangasi ukeni ni muwasho sehemu ya ndani ya uke ambao unaweza kuambatana pia na kuvimba kwa uke. Leo sitaongelea sana juu ya nini kinasababisha hizi fangasi sehemu ya uke bali tutaona dozi kamili ya asili inayoweza kutibu kabisa tatizo hili linalosumbuwa wanawake wengi miaka sasa. Tumia dawa hizi 3 zote kwa pamoja ili kupata matokeo mazuri na usiache kuleta mrejesho hapa namna unavyoendelea: 1. LEMONADE Lemonade inaandaliwa kwa kutumia limau, maji, asali na mdalasini ya unga kidogo, nayo inaandaliwa hivi: *Chukua asali mbichi nusu Lita *Chukua limau kubwa 12 au zaidi, zikate katikati kila moja. Zikamuwe moja baada ya nyingine kupata maji maji ya limau mpaka umepata ujazo wa nusu lita. *Kwenye sufuria nyingine kubwa changanya mdalasini ya unga vijiko vikubwa 10 na maji lita 2 na nusu na uchemshe kama chai kisha ipua na uchuje na usubiri ipowe iwe ya uvuguvugu kidogo. *Sasa changanya pamoja asali nusu lita, juisi au maji maji ya limau nusu lita, maji ya uvuguvugu ya m...

TIBA YA MTU ALIEINGIWA NA JINNI SUGU.

kabla sijatoa tiba yake, ni lazima ujue unatibu nini na kwanini ni jinni. Maana zipo dalili mbalimbali zinazoonyesha mgonjwa amehusudiwa na jini na ni jini aina gani aliemuingilia muhusika. Zifuatazo ni aina na utaratibu wa kumtibu jini sugu. Dawa za kula. Habbatsaudai Habbatsufa Bakahadi Manimani Uzile Habbat rehani Karkam Halilinji Alhamza Kamun aswad Zamda Khardal Daarfilfil Filfil aswad Haltit Zaatar Harmal Sufa nyeupe Manimani Shomari Udinadi Ulinjani Sakabanji Kamun abyadh Uwatu Giligilani Karafuu Tangawizi Mdalasini Maua waridi Hakikisha dawa hizi umezitwanga na kuwa laini kisha utachukua kijiko kimoja cha kila dawa na kuchanganya kwenye asali safi ya nyuki lita moja na uisomee ruqya na mgonjwa awe anakunywa vijiko viwili mara tatu kwa siku kwa mda wa siku 30. NB Hakikisha wakati mgonjwa anatumia dawa za kula ambatanishe na za kujifukiza pamoja na za kujipaka. DAWA ZA KUFUKIZA kiribiti upele Sandarusi Haltit Karafuu maiti Mruturutu ...

KICHOMI

  Kichomi   ni moja ya dalili za ugonjwa moyo. Kupatwa kichomi mara moja moja si vibaya. Ukipatwa muda mrefu au kila wakati ; basi, chunguza zaidi. Kichomi husababishwa au kinaweza kuwa. Dalili ya matatizo ya tumbo lenye asidi (acid) kuzidi Dalili za ugonjwa wa moyo uitwao Ischemic Jambo la kuangalia ni je? Unashikwa kichomi ukiwa unatembea? Umeinama au umelala Ukishakula chakula Kama unapatwa kichomi wakati ukitembea au ukishafanya mazoezi makali ina maana kuna tatizo la damu kuingia sawasawa au kuzunguka (circulation) katika moyo. Kama unapatwa kichomi baada ya kula ina maana kuna tatizo katika chakula unachokula. Je mlo wako una acid(uchachu) sana? Je, unakula vyakula vyenye pilipili na binzari(spices) kwa wingi sana? Kama una kula sana vyakula vyenye asidi ina maana tumbo lako halimeng’enyui sawasawa linachoka. Kawaida binadamu unabidi kubadili badili ulaji. Usirudie vitu fulani fulani kila siku. Mathalan usiweke pilipili katika kila mlo. Tatizo ji...