Skip to main content

BUNSAJI


Leo nataka kupeana faida ndogo kuhusu mafuta yaliyochanganywa na *BUNSAJI.*mafuta haya hufaa sana kwa :-
- kichwa kilicho na harara ukipaka kichwani.
- mafuta hayo huwafaa sana watu ambao hawapati usingizi wakipaka kichwani.
- mafuta hayo hurutubisha ubongo ukipaka kichwani.
- hufaa sana kwa watu wenye uyabisi na kupasuka pasuka ( dandruff ) ukipaka kichwani.
-  hufaa sana kwa mtu anaejikuna sana kichwani.

 *NAMNA YA KUYATENGENEZA.*
chukua bunsaji kisha iponde iwe unga kisha iroweke katika maji unayotaka kuyachemsha masaa 12, baada ya hapo utaichemsha sana mpaka ibaki sawa na mafuta yako unayotaka kuchanganyia kama ni ya nazi, zaituni ama yeyote yale. Kama itakuwa mafuta yako ni nusu lita hakikisha umeichemsha bunsaji mpaka ikafika nusu lita nayo, kisha changanya pamoja baada ya kuichuja na uweke jikoni ichemke mpaka maji yote ya bunsaji yamekauka na kubaki mafuta pekee. Hapo sasa itakuwa tayari kwa matumizi.

Kwa ushauri/tiba ya maradhi mbalimbali wasiliana nami.

Comments

Popular posts from this blog

TIBA YA MTU ALIEINGIWA NA JINNI SUGU.

kabla sijatoa tiba yake, ni lazima ujue unatibu nini na kwanini ni jinni. Maana zipo dalili mbalimbali zinazoonyesha mgonjwa amehusudiwa na jini na ni jini aina gani aliemuingilia muhusika. Zifuatazo ni aina na utaratibu wa kumtibu jini sugu. Dawa za kula. Habbatsaudai Habbatsufa Bakahadi Manimani Uzile Habbat rehani Karkam Halilinji Alhamza Kamun aswad Zamda Khardal Daarfilfil Filfil aswad Haltit Zaatar Harmal Sufa nyeupe Manimani Shomari Udinadi Ulinjani Sakabanji Kamun abyadh Uwatu Giligilani Karafuu Tangawizi Mdalasini Maua waridi Hakikisha dawa hizi umezitwanga na kuwa laini kisha utachukua kijiko kimoja cha kila dawa na kuchanganya kwenye asali safi ya nyuki lita moja na uisomee ruqya na mgonjwa awe anakunywa vijiko viwili mara tatu kwa siku kwa mda wa siku 30. NB Hakikisha wakati mgonjwa anatumia dawa za kula ambatanishe na za kujifukiza pamoja na za kujipaka. DAWA ZA KUFUKIZA kiribiti upele Sandarusi Haltit Karafuu maiti Mruturutu ...

KUONDOSHA MARADHI YA SUBIAN NA KUONDOA WASIWASI

Kwa mtu mwenye matatizo hayo achukue dawa zifuatazo :- - unga wa ambari nyeusi. - unga wa mvuje. - unga wa kitunguu thaum. - mafuta ya uto. - mafuta original ya zaituni. Maelezo Changanya na iwe unajipaka mwili mzima asubuhi na jioni kwa mda wa siku 21.

UTOSI KUINGIA NDANI KWA MTOTO MCHANGA.

chukua manjano mbichi iponde iwe laini sana, kisha chukua pamba na uiweke ile dawa, kisha muekee mtoto mchanga aliena tatizo hilo utosini. In shaa allah utosi utarudi sawa. Utafanya hivyo kwa siku mara moja mpaka tatizo litakapokwisha.