Upungufu wa damu husababishwa
na nini?.
Upungufiu wa damu husababishwa na ukosefu wa madni chuma mwilini (Iron).
Mwili unaitaji madini chuma kwa wingi kwa ajili ya kutengeneza chembe hai nyekundu za damu (red blood cell).
Unapokuwa mjamzito kiwngo cha madini chuma (Iron) yanayotakiwa mwilini huongezeka kutoka 18 milligram kwa siku mpaka 27 milligram kwa siku.
hii ni kutokana na mwili kuhitaji damu nying kwa ajili ya kufanya kazi mbalimbali zinazoongezeka mwilini kwa ajili ya kusapoti ukuaji wa mtoto.
Damu ni muhimu sana kwa mama
mjamzito.
Hivyo basi jitahid kula yakula vyenye kuongeza Damu.
Vyakula vinavyoongeza Damu
vimegawika katika makund mawili
Heme Iron.
hivi ni vyakula ambavyo mwili huweza kuichukua kirahis Iron yake navyo ni Nyama,Samaki,Kuku,Maini na Dagaa.
Pia kuna Non Heme.
hivi ni vyakula ambavyo vina Iron ya
kutosha ila mwil hauwezi kuichukua kirahis hivyo basi unapokula vyakula hivyo jitahid kula vyakula vyenye vitamin C kama Machungwa mapapai Nyanya na hoho ili usaidie kuchukuliwa kwake.
Mfano wa vyakula hivi ni Beetroot Mboga za majani zote hasa
matembele na spinach.Juice ya tembele na passion husaidia kuongeza damu kwa haraka hasa kwa wale ambao beetroot imewashinda,hii juice inaongeza damu kwa haraka sana
Njinsi ya kuandaa.
Osha matembele yako kwenye maji
ya vuguvugu kuondoa uchafu
ukimaliza yakate Kate weka kwa
blender na mbengu za passion
saga na maji,
ukimaliza chuja juice yako japo unaweza kunywa hivyo hivyo au ukaongezea sukari.
Unaweza changanya na ubuyu
mweupe pia badala ya passion
Ubuyu mweupe utatumia juice
yake Kunywa Mara mbili kwa siku kadri uezavyo ladha yake ni nzuri huwezi kushidwa tumia.
Vyakula vingine ni Mayai mayai
ya kienyeji Greenbeans.Maboga
Tambi Viazi vitamu.
Tende unaweza changanya na maziwa fresh Viazi mbatata au viazi ulaya Maharage viazi vitamu njegere ndegu Karanga almond Mbengu za maboga Kunde chemsha kunywa maji yake au supu yake.
Majani ya parachichi,chemsha
kunywa maji yake Unapokula vyakula vyenye Iron usinywe na chai kahawa au soya huzuia (absorbtion)kuchukuliwa kwa madini chuma(Iron).
Pia unapokunywa vidonge vile vya
Damu ulivyopewa clinic baada ya
kumeza unatakiwa ule na Chungwa au Papai viweze kuchukuliwa mwilini kirahisi.
Dalili za kupungukiwa damu kwa
mama mjamzito.
Mama mjamzito unapohisi dalili
zifuatazo ni vizuri kupima wingi
wa damu,kwani kiasi cha damu
kinatakiwa kisiwe chini ya 11g/dL
mpaka mama unapoenda kujifungua
Kuchoka sana,japo kuchoka sana ni hali ya kawaida kwa mama mjamzito,hivyo unapoona unachoka sana ni vizuri kwenda kuangalia wingi wa damu.
kukosa pumzi (breathless).
Kizunguzungu,Maumivu makali ya kichwa.
Miguu kuishiwa nguvu.
Midomo kupauka.
kupata hamu ya kula udongo, ice
(mabarafu ) na vitu vyote
ambavyo sio vyakula.
Angalizo.
mama jitahidi kiwangu cha damu yako kiwe 11g/dL na kuendelea kipindi chote cha ujauzito kwani upungufu wa damu unaweza kusababishwa mtoto akazaliwa na uzito mdogo, kuzaliwa kabla ya muda.