Ni inflamesheni ya tando zinazofunika na kuukinga ubongo na uti wa mgongo , sehemu inayojulikana kwa kijumla kama meninjesi. Inflamisheni hii inaweza kusababishwa na maambukizi ya virusi,bakteria,au na vimelea wengine. (Inflamisheni humaanisha maumivu.) Dalili za meninjitisi zinazotokea mara nyingi ni maumivu ya kichwa na kukazika kwa shingo , hali inayohusishwa na homa , kuchanganyikiwa au ufahamu uliogeuka, kutapika, na kukosa uwezo wa kustahimili mwanga (fotofobia ) au kelele kali ( fonofobia ). Mara nyingi watoto hudhihirisha dalili zisizo mahususi pekee kama vile kizunguzungu na kuwashwa. Uwepo waupele unaweza kuwa dalili ya kisababishi maalumu cha meninjitisi; kwa mfano, meninjitisi inayosababishwa na bakteria aina ya meningokokasi unaweza kuambatana na upele. Kwa watu wazima, dalili ya meninjitisi inayotokea mara nyingi ni maumivu ya kichwa yaliyo makali, ambayo hutokea kwa karibu asilimia 90 ya visa vya meninjitisi ya kibakteria,ambavyo hufuatwa na ku...