Skip to main content

Posts

KUVIMBA MWILI

Assalamu alaikum  Kwa mtu mwenye tatizo kama hili anatakiwa achukue kamun (bizari ile inayopikiwa pilau ) na karawiya kiingereza inaitwa caraway. Hakikisha kila moja ni ujazo sawa na ponda iwe unga laini. Kisha tia kijiko kimoja cha unga huo kwa Maji vuguvugu glass moja na unywe yote. Hakikisha unakunywa asubuhi kabla hajakula kitu kwa mda wa siku 30. In shaa llah utapona. Kwa tiba ya aina yeyote wasiliana nami.

KUVIMBA MIGUU KWA MJAMZITO.

Akina mama wengi huwa wanapata matatizo ya kuvimba miguu wakati wa ujauzito kwa sababu mbalimbali. Wengine huwa ni kawaida kwa maana ya kwamba haisababishwi na ugonjwa wa aina yoyote. Wakati mimba inapokua kubwa huweza tumbo la uzazi Uterus hukandamiza mishipa ya damu inayorudisha damu kwenye moyo Veins au ile mishipa inayobeba maji damu lymph kutoka kwenye miguu. Hali hiyo hufanya damu na hayo maji damu kushindwa kurudi yote kwenye moyo na kujikusanya sehemu ambazo ni Dependent hasa miguuni na kusababisha uvimbaji wa miguu Dependent Oedema. Uvimbaji huu ni ule ambao sana uko kwenye sehemu ya mguu chini ya kifundo cha mguu Ankle Oedema, kama miguu ikivimba kupanda juu hadi kwenye mapaja au juu zaidi hii huwa ni dalili ya ugonjwa. Magonjwa ambayo yanaweza kusababisha uvimbe miguuni na sehemu nyingine za mwili wa mjamzito ni pamoja na kuwa na shinikizo la damu la ujauzito Pre-eclampsia, magonjwa ya figo ambapo mtu huvimba miguu, uso pia, magojwa ya ini – haya husababisha p...

TIBA YA ASILI YA FANGASI UKENI.

Fangasi ukeni ni muwasho sehemu ya ndani ya uke ambao unaweza kuambatana pia na kuvimba kwa uke. Leo sitaongelea sana juu ya nini kinasababisha hizi fangasi sehemu ya uke bali tutaona dozi kamili ya asili inayoweza kutibu kabisa tatizo hili linalosumbuwa wanawake wengi miaka sasa. Tumia dawa hizi 3 zote kwa pamoja ili kupata matokeo mazuri na usiache kuleta mrejesho hapa namna unavyoendelea: 1. LEMONADE Lemonade inaandaliwa kwa kutumia limau, maji, asali na mdalasini ya unga kidogo, nayo inaandaliwa hivi: *Chukua asali mbichi nusu Lita *Chukua limau kubwa 12 au zaidi, zikate katikati kila moja. Zikamuwe moja baada ya nyingine kupata maji maji ya limau mpaka umepata ujazo wa nusu lita. *Kwenye sufuria nyingine kubwa changanya mdalasini ya unga vijiko vikubwa 10 na maji lita 2 na nusu na uchemshe kama chai kisha ipua na uchuje na usubiri ipowe iwe ya uvuguvugu kidogo. *Sasa changanya pamoja asali nusu lita, juisi au maji maji ya limau nusu lita, maji ya uvuguvugu ya m...

BUNSAJI

Leo nataka kupeana faida ndogo kuhusu mafuta yaliyochanganywa na *BUNSAJI.*mafuta haya hufaa sana kwa :- - kichwa kilicho na harara ukipaka kichwani. - mafuta hayo huwafaa sana watu ambao hawapati usingizi wakipaka kichwani. - mafuta hayo hurutubisha ubongo ukipaka kichwani. - hufaa sana kwa watu wenye uyabisi na kupasuka pasuka ( dandruff ) ukipaka kichwani. -  hufaa sana kwa mtu anaejikuna sana kichwani.  *NAMNA YA KUYATENGENEZA.* chukua bunsaji kisha iponde iwe unga kisha iroweke katika maji unayotaka kuyachemsha masaa 12, baada ya hapo utaichemsha sana mpaka ibaki sawa na mafuta yako unayotaka kuchanganyia kama ni ya nazi, zaituni ama yeyote yale. Kama itakuwa mafuta yako ni nusu lita hakikisha umeichemsha bunsaji mpaka ikafika nusu lita nayo, kisha changanya pamoja baada ya kuichuja na uweke jikoni ichemke mpaka maji yote ya bunsaji yamekauka na kubaki mafuta pekee. Hapo sasa itakuwa tayari kwa matumizi. Kwa ushauri/tiba ya maradhi mbalimbali wasiliana nami.

ALMONDS/LOZI

leo ndugu zangu nataka kuzungumzia faidia cheche zitokanazo na tunda hili. watu wengi wamelichukulia tunda hili huliwa na watu wenye maradhi ama wenye hela zao. Ila kwa ushauri nawaomba tukumbatie tunda hili kwa wingi maana lina faida nyingi sana. Hizi ni baadhi ya faida ya tunda hili:- - husafisha tumbo. - huongeza maziwa mengi kwa wanyonyeshaji. - kusaidia sana kwa wenye maradhi ya mishipa/nerves. - husaidia sana kwa watu wenye maradhi ya kibofu cha mkojo. - lozi ni nzuri sana kwa mtu mwenye maradhi ya figo. - ni nzuri sana kwa wenye maradhi ya kisukari. - hufungua njia za mkojo. - lozi hutia nguvu ubongo hasa kwa wenye kusahau sahau na udhaifu wa kumbukumbu. - mafuta yake ni mazuri kwa mtu mwenye maradhi ya ngozi hutibu. - mafuta yake ni mazuri kwa mtu aliepooza, hutibu. - mafuta yake ni mazuri kwa mtu aliyechomeka ngozi, hutibu. - lozi husaidia kwa mtu mwenye uchache wa mbegu za kiume. NB tunda hili linatibu maradhi mengi sana. Kwa ushauri/tiba wasiliana nami...

Tatizo la mimba kutunga nje ya mfuko wa uzazi (ectopic pregnancy)

Mimba kutunga nje ya mfuko wa uzazi wa mwanamke au ectopic pregnancy ni tatizo ambalo limetokea kuathiri wanawake mbalimbali. Kwa kawaida, isipokuwa mara chache sana, mimba zitungazo nje ya mfuko wa uzazi hazina uwezo wa kukua kuwa mtoto kamili. Aidha, mimba hizi ni hatari kwa afya ya mama mjamzito kwa vile humfanya kupoteza damu nyingi na hatimaye kusababisha kifo. Nini hutokea?. Kazi za mirija ya fallopian ni kusafirisha mayai kutoka katika kiwanda chake cha uzalishaji (ovary) mpaka kwenye mfuko wa uzazi (uterus). Utungisho wa yai la kike (ovum) na mbegu ya kiume (sperm) hufanyika kwenye mirija hii. Mara baada ya utungisho, misuli inayozunguka mirija ya fallopian ikishirikiana na vinyweleo vilivyopo ndani ya mirija hii husukuma kiinitete au yai lililorutubishwa kulipeleka kwenye uterus. Yai lililorutubishwa, au kiinitete, lifikapo kwenye uterus hujipachika katika mojawapo ya kuta zake kwa ajili ya kuendelea kurutubishwa, kukua taratibu na hatimaye kufanya mtot...

DEGEDEGE

Degedege Ni Nini ? Ni hali ya ghafla ya kutingishika kwa mwili mzima au miguu na mikono,ambayo husababishwa na kukakamaa kwa misuli ya mwili. Hali hii uhusishwa na magonjwa ya ubongo kama kifafa,vichocheo vya kwenye damu kama upungufu wa sukari(hypoglycemia), upungufu wa oxygen(hypoxia),kushuka kwa shinikizo la damu(hypotension) na maambukizi na homa ya degedege. Homa ni Nini ?. Ni hali ya kawaida ya mwili kushindwa kujikinga na maambukizi. Na kwa watoto hutokea pale joto la mwili linapokuwa zaidi ya nyuzi 38 za sentigredi. Homa ya Degedege Ni Nini ?. Ni degedege linalotokea kwa watoto ghafla likiambatana na homa kali iliyotokana na kuongezeka haraka kwa joto la mwili. Ugonjwa huu utokea kwa wastani wa asilimia nne (4%) ya watoto walio kati ya umri wa miezi sita na miaka mitano. Watoto wengi ambao hupatwa na ugonjwa huu huwa haiwapelekei baadae kuwa na matatizo ya kudumu kama kupata ugonjwa wa kifafa,niasilimia tatu (3%) tu ambao wanaweza baadae kupata ugonjwa w...