Skip to main content

Tatizo la mimba kutunga nje ya mfuko wa uzazi (ectopic pregnancy)




Mimba kutunga nje ya mfuko wa uzazi wa mwanamke au ectopic pregnancy ni tatizo ambalo limetokea kuathiri wanawake mbalimbali.

Kwa kawaida, isipokuwa mara chache sana, mimba zitungazo nje ya mfuko wa uzazi hazina uwezo wa kukua kuwa mtoto kamili.


Aidha, mimba hizi ni hatari kwa afya ya mama mjamzito kwa vile humfanya kupoteza damu nyingi na hatimaye kusababisha kifo.


Nini hutokea?.

Kazi za mirija ya fallopian ni kusafirisha mayai kutoka katika kiwanda chake cha uzalishaji (ovary) mpaka kwenye mfuko wa uzazi (uterus).


Utungisho wa yai la kike (ovum) na mbegu ya kiume (sperm) hufanyika kwenye mirija hii.


Mara baada ya utungisho, misuli inayozunguka mirija ya fallopian ikishirikiana na vinyweleo vilivyopo ndani ya mirija hii husukuma kiinitete au yai lililorutubishwa kulipeleka kwenye uterus.


Yai lililorutubishwa, au kiinitete, lifikapo kwenye uterus hujipachika katika mojawapo ya kuta zake kwa ajili ya kuendelea kurutubishwa, kukua taratibu na hatimaye kufanya mtoto.


Inapotokea misuli hii kushindwa kufanya kazi au vinyweleo hivi kukosekana, kiinitete hushindwa kusafirishwa kuingia kwenye uterus na hivyo hujitunga nje ya uterus kusababisha ectopic pregnancy.


Karibu asilimia 1-2% ya mayai yaliyorutubishwa hutunga nje ya mfuko wa uzazi wa mwanamke.

Aidha, zaidi ya asilimia 95% ya mimba zinazotunga nje ya uterus hutokea kwenye mrija wa fallopian.


Mimba zinazotunga kwenye mrija wa fallopian husababisha kiinitete (embryo) kujipachika katika kuta zake na hivyo kusababisha mishipa ya damu inayopita karibu na mrija wa fallopian kupasuka na damu kutoka kwa wingi hali ambayo isiposhughulikiwa mapema husababisha madhara zaidi na hata kifo.


Aina za Ectopic Pregnancy.

Kuna aina kuu nne za mimba zinazotunga nje ya mfuko wa uzazi, nazo ni.


1.Mimba zinazotunga kwenye mirija ya fallopian.

2.Mimba zinazotunga nje ya uterus na nje mirija ya fallopian.

3.Mimba zinazotunga ndani na nje ya uterus kwa wakati mmoja.

4.Mimba zinazojirudia kutunga nje ya mfuko wa Uzazi


👉Mimba zinazotunga kwenye mirija ya fallopian.

Sababu kubwa inayopelekea mimba kutunga kwenye mirija ya fallopian ni kushindwa kusafirishwa kwa kiinitete katika mirija hii hali inayotokana na mabadiliko katika hali ya mirija au uwezo duni wa mirija hiyo katika kusukuma kiinitete kuingia kwenye uterus kwa sababu ya ukosefu wa vinyweleo kutokana na magonjwa mbalimbali yanayoathiri muundo na maumbile ya mirija ya fallopian.


Mimba zinazotunga kwenye mirija ya fallopian huwa zina madhara makubwa zaidi kwa sababu eneo hili ni jembamba mno kuweza kuhimili ukuaji wa mimba na pia lina mishipa mingi ya damu inayopita karibu ambayo ipo hatarini kupasuka hivyo kupelekea mgonjwa kupoteza damu nyingi sana.


👉Mimba zinazotunga nje ya uterus na nje mirija ya fallopian.

Baadhi ya mimba huweza kutunga kwenye kiwanda cha kuzalisha mayai (ovary), kwenye shingo ya uzazi (cervix) au ndani ya tumbo (intra-abdominal).


Aina hii ya mimba ni chini ya asilimia tano ya mimba zote zinazotunga nje ya mfuko wa uzazi.


👉Mimba inayotungwa ndani ya tumbo (intra-abdominal)

wakati fulani huweza kutoa mtoto aliye hai tofauti na aina nyingine za mimba zinazotunga nje ya uterus.

Hata hivyo uzalishaji wake hufanywa kwa operesheni ingawa hakuna ushahidi wa kitabibu kuhusu suala hili mpaka sasa.


Madhara ya kutokea kwa upotezaji wa damu pamoja na maambukizi ni makubwa hivyo mara nyingi mimba za namna hii huitaji kushughulikiwa haraka ili kumuepushia madhara makubwa mama mjamzito.


👉Mimba zinazotunga ndani na nje ya uterus kwa wakati mmoja.

Wakati fulani, mayai mawili yaliyorutubishwa kwa wakati mmoja hutokea kupandikizwa sehemu mbili tofauti.

Moja likipandikizwa nje ya uterus na jingine ndani ya uterus.

Katika aina hii ya ectopic pregnancy, uwezekano wa yai lililotungwa ndani ya uterus kukua na kutoa mtoto ni mkubwa sana.


👉Mimba zinazojirudia kutunga nje ya mfuko wa Uzazi.

Wakati fulani hutokea kuwa, hata baada ya operesheni ya kuondoa mimba iliyotunga nje ya kizazi kufanyika, baada ya muda fulani seli za kiinitete huendelea kukua na kujitengeneza tena kufanya kusanyiko la seli kama mimba nyingine.

Hali hii huitwa mimba zinazoendelea kutunga nje ya mfuko wa uzazi au persistent ectopic pregnancy.


Nini husababisha mimba kutunga nje ya kizazi?

Katika mimba nyingi zinazotunga nje ya uterus, chanzo chake huwa hakijulikani.

Hata hivyo kuna vihatarishi ambavyo humfanya mwanamke kuwa katika hatari ya kupata tatizo hili. Vihatarishi hivi ni pamoja na.

1.Matatizo katika mirija ya fallopian
Magonjwa yanayoweza kusababisha hali hii ni pamoja na.

·Maambukizi katika mfumo wa uzazi wa mwanamke (PID).

·Matumizi ya vitanzi vya kuzuia mimba (Intra-uterine contraceptive devices).

·Kuoteana kwa tishu za uterus kwenye viungo vingine vya uzazi au endometriosis.


2.Uvutaji sigara.

Uvutaji sigara kwa mwanamke una uhusiano mkubwa na utungaji wa mimba nje ya kizazi.

Imeonekana kwamba wanaowake wanaopendelea kuvuta sigara mara kwa mara wana hatari ya kupatwa na tatizo hili mara tano zaidi ya wale wasiovuta kabisa.

Hali hii husababishwa na nicotini iliyomo ndani ya tumbaku. Kwa kawaida nicotini huchochea kusinyaa kwa mirija ya fallopian hali iletayo kuziba kwa mirija hiyo na hivyo kufanya kiinitete kushindwa kupita kwenye mirija kuingia kwenye uterus na kufanya mimba kutunga kwenye mirija ya fallopian.


3.Upasuaji wa tumbo uliofanyika zamani.

Operesheni yeyote inayohusu mirija ya fallopian inaongeza uwezekano wa mwanamke kutunga mimba nje ya uterus kwa vile mirija ya fallopian huwa imesinyaa kutokana na operesheni hiyo.


4.Matumizi holela ya baadhi ya dawa.

Matumizi ya baadhi ya dawa zenye homoni husababisha kupungua kwa uwezo wa mirija ya fallopian kusukuma kiinitete kuelekea kwenye uterus na hivyo kuleta uwezekano wa utungaji wa mimba nje ya kizazi.


Dawa hizo ni kama dawa za kuzuia mimba zenye homoni za kike za progesterone, na dawa za kusaidia uzazi aina ya clomiphene.


👉Dalili za ectopic pregnancy.

Katika wiki za mwanzo za ujauzito, mimba iliyotunga nje ya uterus huwa na dalili sawa na za mimba ya kawaida.

Dalili hizi ni pamoja na mwanamke kukosa hedhi, kujaa kwa matiti, kichefuchefu, na uchovu wa mwili.


Hali hii hufanya ugunduzi wa mimba iliyotunga nje ya uterus kuwa mgumu katika hatua zake za awali.

Hata hivyo dalili ya awali ya kuonesha kuwa mimba imetunga nje ya kizazi ni kuwepo kwa maumivu makali na damu kutoka ukeni.

Maumivu yanaweza kuwa kwenye nyonga, tumbo au wakati mwingine kwenye mabega au shingo (iwapo kiwango cha damu inayotoka kwenye mirija iliyopasuka ni kingi sana mpaka kugusa kiwambo cha hewa).

Maumivu haya huweza kuwa makali na yanayokata kama kisu, na yanaweza kuwa upande mmoja zaidi wa nyonga ingawa si lazima yawe upande ulio na mimba.

Dalili nyingine ni pamoja na.

·Kizunguzungu na kuzimia kwa sababu ya kupoteza damu kwa wingi.

·Shinikizo la damu kuwa chini, na
·Maumivu ya chini ya mgongo


Ugunduzi wa ectopic pregnancy.

Mimba iliyotungwa nje ya kizazi huweza kugunduliwa kwa Daktari kusikiliza historia ya mgonjwa na kufahamu dalili zake na kumfanyia uchunguzi wa mwili (physical examination).

   
·Kufanya vipimo kadhaa vinavyoonesha kuwepo kwa tatizo hilo.

Vipimo hivyo ni pamoja na
·Kupima damu kwa ajili ya kuangalia kiwango cha homoni ya HCG.

·Kupima kiwango cha homoni ya progesterone ambayo kwa mama mwenye ectopic pregnancy huwa chini (chini ya 15ng/mls) zaidi ya mwenye mimba ya kawaida.


·Ultrasound ambayo husaidia kutambua mimba ilipotungwa.


Matibabu ya Ectopic pregnancy
Matibabu ya mimba iliyotunga nje ya kizazi yaweza kuwa ya aina mbili, yale yasiyohitaji upasuaji, au yanayohitaji uangalizi na dawa na yale yanayohitaji upasuaji.

Popular posts from this blog

TIBA YA ASILI YA FANGASI UKENI.

Fangasi ukeni ni muwasho sehemu ya ndani ya uke ambao unaweza kuambatana pia na kuvimba kwa uke. Leo sitaongelea sana juu ya nini kinasababisha hizi fangasi sehemu ya uke bali tutaona dozi kamili ya asili inayoweza kutibu kabisa tatizo hili linalosumbuwa wanawake wengi miaka sasa. Tumia dawa hizi 3 zote kwa pamoja ili kupata matokeo mazuri na usiache kuleta mrejesho hapa namna unavyoendelea: 1. LEMONADE Lemonade inaandaliwa kwa kutumia limau, maji, asali na mdalasini ya unga kidogo, nayo inaandaliwa hivi: *Chukua asali mbichi nusu Lita *Chukua limau kubwa 12 au zaidi, zikate katikati kila moja. Zikamuwe moja baada ya nyingine kupata maji maji ya limau mpaka umepata ujazo wa nusu lita. *Kwenye sufuria nyingine kubwa changanya mdalasini ya unga vijiko vikubwa 10 na maji lita 2 na nusu na uchemshe kama chai kisha ipua na uchuje na usubiri ipowe iwe ya uvuguvugu kidogo. *Sasa changanya pamoja asali nusu lita, juisi au maji maji ya limau nusu lita, maji ya uvuguvugu ya m...

TIBA YA MTU ALIEINGIWA NA JINNI SUGU.

kabla sijatoa tiba yake, ni lazima ujue unatibu nini na kwanini ni jinni. Maana zipo dalili mbalimbali zinazoonyesha mgonjwa amehusudiwa na jini na ni jini aina gani aliemuingilia muhusika. Zifuatazo ni aina na utaratibu wa kumtibu jini sugu. Dawa za kula. Habbatsaudai Habbatsufa Bakahadi Manimani Uzile Habbat rehani Karkam Halilinji Alhamza Kamun aswad Zamda Khardal Daarfilfil Filfil aswad Haltit Zaatar Harmal Sufa nyeupe Manimani Shomari Udinadi Ulinjani Sakabanji Kamun abyadh Uwatu Giligilani Karafuu Tangawizi Mdalasini Maua waridi Hakikisha dawa hizi umezitwanga na kuwa laini kisha utachukua kijiko kimoja cha kila dawa na kuchanganya kwenye asali safi ya nyuki lita moja na uisomee ruqya na mgonjwa awe anakunywa vijiko viwili mara tatu kwa siku kwa mda wa siku 30. NB Hakikisha wakati mgonjwa anatumia dawa za kula ambatanishe na za kujifukiza pamoja na za kujipaka. DAWA ZA KUFUKIZA kiribiti upele Sandarusi Haltit Karafuu maiti Mruturutu ...

KICHOMI

  Kichomi   ni moja ya dalili za ugonjwa moyo. Kupatwa kichomi mara moja moja si vibaya. Ukipatwa muda mrefu au kila wakati ; basi, chunguza zaidi. Kichomi husababishwa au kinaweza kuwa. Dalili ya matatizo ya tumbo lenye asidi (acid) kuzidi Dalili za ugonjwa wa moyo uitwao Ischemic Jambo la kuangalia ni je? Unashikwa kichomi ukiwa unatembea? Umeinama au umelala Ukishakula chakula Kama unapatwa kichomi wakati ukitembea au ukishafanya mazoezi makali ina maana kuna tatizo la damu kuingia sawasawa au kuzunguka (circulation) katika moyo. Kama unapatwa kichomi baada ya kula ina maana kuna tatizo katika chakula unachokula. Je mlo wako una acid(uchachu) sana? Je, unakula vyakula vyenye pilipili na binzari(spices) kwa wingi sana? Kama una kula sana vyakula vyenye asidi ina maana tumbo lako halimeng’enyui sawasawa linachoka. Kawaida binadamu unabidi kubadili badili ulaji. Usirudie vitu fulani fulani kila siku. Mathalan usiweke pilipili katika kila mlo. Tatizo ji...