Skip to main content

Posts

KUFUNGUA HEDHI

assalamu alaikum, Leo nipeonelea kutoa mada hii maana tatizo hili linawakumba wanawake mbali mbali kwasababu mbali mbali ikiwemo 1. Hormone imbalanced 2. Utumiaji wa dawa za upangaji uzazi. 3. Matatizo ya kijini. Na matatizo mengineo mengi tu. Kwa mtu mwenye tatizo kama hili ana takiwa kwanza ajue tatizo husika ndiposa apate tiba muafaka ili shida imuondokee. Ifuatayo ni tiba ya mtu mwenye tatizo kama hili kwa upande hormone imbalance :- Chukua haltit kijiko kimoja, fulfil abyadh kijiko kimoja, siki kikombe cha chai na Maji Lita moja. Changanya vyote pamoja na iwe unakunywa nusu kikombe kutwa Mara mbili kwa mda wa siku 14. Kwa tiba na ushauri usisite kuwasiliana nami kwa +254732917064.

MAMBO YAKUFANYA ILI MIMBA IWE SALAMA

Kulingana na Hazina ya Umoja wa Mataifa ya Idadi ya Watu,zaidi ya wanawake nusu milioni hufa kila mwaka kutokana na matatizo yanayohusiana na mimba. Isitoshe,Shirika la Umoja wa Mataifa la Hazina ya Watoto linasema kwamba kila mwaka zaidi ya wanawake milioni 60 huugua vibaya wakiwa wajawazito hivi kwamba karibu thuluthi moja kati yao hupata majeraha au maambukizo yanayodumu muda mrefu.     Katika nchi zinazoendelea, wanawake wengi hupata mimba moja baada ya nyingine,hujifungua, na kujiachilia, jambo ambalo huwafanya wawe wachovu na wagonjwa. mimba inaweza kuleta madhara hata kuhatarisha uhai.       JE, MWANAMKE ANAWEZA KUFANYA NINI ILI MIMBA YAKE IWE SALAMA ZAIDI ?   Utunzaji wa Kiafya Kabla ya Kuwa  Mjamzito. 1.Kupanga.  Huenda waume na wake wakahitaji kuzungumza kuhusu idadi ya watoto ambao watapata. Katika nchi zinazoendelea,ni kawaida kuwaona wanawake wenye watoto wanaonyonya wakiwa wajawazito. K...

HIATUS HERNIA (NGIRI YA KIFUA)

Hiatus Hernia   ni tundu linalotokea baada ya sehemu ya juu ya mfuko wa kuhifadhia chakula (tumbo) kuingia kwenye sehemu ya kifua kupitia uwazi unaojulikana kama   esophageal hiatus . Kwa kawaida uwazi huu   (esophageal hiatus)   hupitisha mrija wa chakula kwenda kwenye tumbo yaani   esophagus   na si utumbo. Mara nyingi, tatizo hili huonekana kwa takribani ya 60% ya watu wenye umri wa miaka 50 na kuendelea, ingawa pia linaweza kuwapata wale walio na umri wa chini ya huo. Kuna aina mbili kuu za hiatus hernia Sliding type :  Kama jina lake linavyomaanisha, aina hii hutokea iwapo sehemu ya juu ya utumbo inaposukumwa juu na kuingia kwenye upenyo wa  esophagus hiatus  baada ya kutokea kwa ongezeko la presha katika maeneo ya tumbo  (increased pressure in the abdominal cavity)  na kurudi kama kawaida wakati presha inapopungua. Fixing type : Aina hii hutokea iwapo sehemu ya juu ya utumbo inapoku...

UDHAIFU WA MBEGU ZA KIUME

Kama kila ukifanya tendo la ndoa, mwanamke anatoka shahawa/mbegu dakika chache mara baada ya kumaliza tendo la ndoa hata kama hajasimama. Iyo ni dalili mojawapo mbegu za kiume sio bora - soma hadi mwisho mada hii nzuri ili kujua kiundani na suluhisho. UBORA WA MBEGU ZA KIUME (SPERM ANALYSIS). Kawaida kazi ya kiuchunguzi wa UBORA WA MBEGU ZA KIUME hufanyika katika hospitali ambapo mbegu zako za kiume huchukuliwa na kisha kuchunguzwa na daktari mzoefu. Unaweza fanya tendo la ndoa kila siku za hatari na bado usitungishe mimba. Tatizo linaweza kuwa kwa mama au baba au wote wawili.Tumesha yaelezea sana matatizo haya katika mada nyingi ziilizopita hapahapa. Kwa upande wa baba kuna wakati unaweza JITAMBUA KAMA huna mbegu bora kutokana na muonekano wa manii/shahawa zako pamoja na kiasi cha shahawa kinachotoka katika kila tendo moja. SOMA HAPA ILI UJIFUNZE MACHACHE. 1.UWINGI WA MBEGU ZA KIUME: Mbegu za kiume katika kila tendo kamilifu moja linalofanywa zinatakiwa zis...

ASTHMA/PUMU

Leo nataka kutoa tiba ya ASTHMA/PUMU. Tiba hii unaweza kujifanyia wewe mwenyewe. Chukua tembe tano za karafuu na utie kwenye sufuria yenye maji kikombe kimoja, chemsha mpaka ibaki nusu kikombe. Kisha chuja na utie asali safi kijiko kimoja baada ya kupoa. Baada ya hapo kunywa yote kwa mara moja. Utafanya zoezi hili mara mbili kwa siku. Inshaallah utapona.

UCHAFU UNAOTOKA UKENI

Uke wa mwanamke hufanya kazi ya kutoa njia kati ya sehemu ya nje ya mwili na viungo vya uzazi vya ndani vya mwanamke. Hali ya kawaida ya majimaji yaliyomo katika uke wa mwanamke huwa ni ya tindikali ili kuzuia maambukizi ya vijidudu wa kuleta maradhi. Hali hii ya utindikali huletwa na bacteria waishio katika uke wa mwanamke. Bacteria hawa ni wa kawaida na hawana madhara kwa mwili. Uke ulio katika hali nzuri hutoa majimaji haya ili kujisafisha. Majimaji haya yanayotengenezwa katika uke na kwenye eno la cervix hufanya kazi ya kuondoa seli zilizokufa na bacteria waharibifu nje ya mwili na huu ndio uchafu wa kawaida ambao mwanamke hutoa ukeni. Kutoa uchafu huu sehemu za siri ni njia ya kuusafisha uke na kuzuia maambukizi ya magonjwa. Kitu cho chote ambacho kitaharibu uwiano wa utengeneaji wa majimaji haya ndani ya uke kinaweza kujenga mazingira ya maambukizi katika uke. Uchafu Wa Sehemu Za Siri Ulio Wa Kawaida Wanawake wote hutoa uchafu sehemu za s...

UCHI KULEGEA

Jee, wewe ni mmojawapo wa wale wanawake wanaohisi kuwa na tatizo la uchi kulegea? Haupo peke yako, wanawake wengi wanatatizwa na jambo hili, wanaweza kuwa wameambiwa jambo hili na wapenzi wao au wao wenyewe walijaribu kujipima kwa kujiingiza vidole kwenye sehemu hizo za siri. Katika makala hii natumia neno uchi, ambalo si neno sahihi sana, nikimaanisha sehemu ya nyeti za mwanamke ambayo hutumika wakati wa kufanya mapenzi, kupitisha damu chafu wakati wa siku za hedhi na kupitisha mtoto wakati anapozaliwa. Neno sahihi ni Kuma. Nalitumia neno hilo kukudhi haja ya wengi waliolizoea. Maneno mengine ambayo yamezoeleka kueleza tatizo hilo ni uchi mpana, uchi mkubwa na mengineyo. Dalili Za Uchi Kulegea Kabla ya yote tutazame uchi huu ulivyoumbwa. Uchi ni kama kijimfuko kirefu kilichozungukwa na misuli ambacho kwa ndani kimezungukwa na utando laini unaovutika wenye unyevunyevu unaosaidia kupunguza msuguano na wenye uwezo wa kuleta hisia za mapenz...