Skip to main content

UDHAIFU WA MBEGU ZA KIUME

Kama kila ukifanya tendo la ndoa,
mwanamke anatoka shahawa/mbegu dakika chache mara baada ya kumaliza tendo la ndoa hata kama hajasimama.

Iyo ni dalili mojawapo mbegu za kiume sio bora - soma hadi mwisho mada hii nzuri ili kujua kiundani na suluhisho.

UBORA WA MBEGU ZA KIUME (SPERM ANALYSIS).

Kawaida kazi ya kiuchunguzi wa
UBORA WA MBEGU ZA KIUME
hufanyika katika hospitali ambapo
mbegu zako za kiume huchukuliwa na kisha kuchunguzwa na daktari mzoefu.

Unaweza fanya tendo la ndoa kila siku za hatari na bado usitungishe mimba.

Tatizo linaweza kuwa kwa mama au baba au wote wawili.Tumesha yaelezea sana matatizo haya katika mada nyingi ziilizopita hapahapa.

Kwa upande wa baba kuna wakati unaweza JITAMBUA KAMA huna mbegu bora kutokana na
muonekano wa manii/shahawa zako
pamoja na kiasi cha shahawa
kinachotoka katika kila tendo moja.

SOMA HAPA ILI UJIFUNZE MACHACHE.

1.UWINGI WA MBEGU ZA KIUME:

Mbegu za kiume katika kila tendo
kamilifu moja linalofanywa zinatakiwa zisispungue milioni 40. Kiasi hiki sio rahisi kukijua kwa macho yako.Lakini ikiwa utatoa shahawa kidogo, kuna uwezekano wa kuwa na mbegu za kiume chache.Ingawa sio mara zote
utoapo shahawa chache basi
humaanisha una mbegu chache.

Mshindo dhaifu au kufika kileleni kirahisi rahisi ni mojawapo ya dalili ya kwamba mbegu unazotoa sio nyingi, inaweza kuwa na maji mengi badala ya kuwa na mbegu nyingi.

2.UZITO WA MBEGU ZA KIUME NA
UWEZO WA KUCHELEWA
KUYEYUKA.

Shahawa/majimaji ya mbegu huwa na mbegu za kiume, na shahawa ni
majimaji yanayobeba mbegu za
kiume, kazi ya shahawa ni kusafirisha kwa usalama mbegu za kiume mpaka kulifikia yai. Sasa ikiwa shahawa zitakuwa nyepesi (zina yeyuka haraka)basi maana yake kwa haraka sana baada ya kutoka uumeni shahawa na mbegu za kiume zinatengana, na hivyo
kuathiri uwezo wa mbegu kusafiri
haraka na kulifikia yai.Mfano mdogo ni kwamba kama ukishafanya kitendo cha ndoa na kisha muda huohuo mbegu za kiume kuanza kuchuruzika kutoka nje
ya uke hata kama mwanamke amelala basi hiyo ni dalili mojawapo ya mbegu kuwa nyepesi na hivyo kuweza kuathiri uwezo wa kutungisha mimba.

Kunaweza kuwa na matatizo mengine ya uko kutoweza kushikilia vizuri mbegu za kiume pia, hiyo nayo inaweza kuwa sababu

3.UWEZO WA KUOGELEA KWA
KWENDA MBELE.

Mbegu za kiume zenye afya bora zinakichwa kikubwa
kilichochongoka na mkia mrefu unao anza mkubwa kichwana na kuishia mdogo kabisa mkiani, sifa hizi zinazipa mbegu uwezo wa wa kuogelea kwenda mbele katika mstari mnyoofu, ikiwa mbegu ya kiume itasafiri katika mstari
wa zigzig au maumboumbo basi
inapoteza uwezo wa kufika haraka
kuliwahi yai. Hii ni kwa sababu
zinachoka. Mbegu zinazoenda katika mstari mnyoofu zinawahi kufika kwa kuwa safari inakuwa fupi. Mfano mzuri ukisafiri na ndege toka Mwanza hadi Dar na Mwingine Asafiri na Train na mwingine na Bas utakuta wanafika muda tofauti na pia wanakuwa wamesafiri umbali tofauti kabisa.Ndivyo ilivyo kwa mbegu zinazoogelea kwa mwendo wa nyoka na zile zinazoogelea kwa kwenda mbele moja kwa moja.

4.UWEZO WA KUISHI.

Mbegu bora inafaa iishi sio chini ya masaa 72 tangia itoke kwa mwanaume na kuingia kwa
mwanamke, maisha mafupi ya mbegu yanaifanya mbegu kuwa na wakati mgumu wa kuliwahi yai ili kulitungisha mimba.

5.RANGI.

Kawaida shahawa zenye mbegu bora zina rangi nyeupe inayoelekea kwenye gray na kwa wazee inakuwa nyeupe inaelekea njano.Sasa huwezi ona rangi hii mara kwa mara
kwa sababu mbalimbali za kiafya,
chakula na hali ya hewa. Lakini kwa
watu wazima miaka 40 kwenda juu ni kawaida sana mara nyingi kuonekana nyeupe/njano.

NINI CHA KUFANYA IKIWA UNAONA
DALILI HIZI ?.

Ukiona dalili hizi au kama umepima na kukutwa na dalili hizi, na ikiwa katika ndoa yako upatikanaji wa mimba imekuwa ngumu, na ikiwa pia mama mara kwa mara hujikuta na mbegu za kiume zinamtoka na kuchuruzika muda mchache mara baada ya tendo la ndoa basi tambua ya kwamba ubora wa mbegu zako ni mdogo na kwa iyo unahitaji utatuzi wake.

KWANZA BORESHA MBEGU ZAKO
ZA KIUME.

kwa kula chakula chenye zinki
kwa wingi mfano mbegu zote za
matunda na maboga zinazolika, zina
zinki na madini ya chuma kwa wingi.Hakikisha hukosi hizo mara kwa mara,ikiwa umeathirika zaidi au tuseme umetumia muda mrefu zaidi ya mwezi na huoni mabadiliko basi huna budi kupata dawa za Asili au kupata virutubisho na madini kutoka katika wasambazaji walio thibitishwa.

PILI ACHANA NA TABIA MBAYA
ZINAZOWEZA KUWA SABABU YA
MBEGU KUWA DHAIFU.

mfano ulevi,sigara, madawa ya kulevya,punyeto, ngono kinyume na
maumbile,kutokula chakula vizuri,
madawa ya kulevya na kukosa kufanyamazoezi ya mara kwa mara.

TATU JITIBU MAGONJWA SUGU.

Huu umekuwa wimbo wa taifa, Magonjwa ya kitabia kama kisukari, presha na matatizo ya ini na figo ni kiashiria tosha ya kwamba mifumo ya mwili imechoshwa na kuzeeshwa na vyakula vibaya tunavyokula. Kwa hivyo ni muhimu kujitibu magonjwa hayo haraka.

NNE CHAKULA BORA NA CHENYE
LISHE ASILI NI MUHIMU.

Kula chakula cha asili na pia mara kwa mara ili uweze kuziba pengo la madini na vitamin unalolikosa kwa sababu ya kula chakula cha ovyo.

Comments

Popular posts from this blog

TIBA YA ASILI YA FANGASI UKENI.

Fangasi ukeni ni muwasho sehemu ya ndani ya uke ambao unaweza kuambatana pia na kuvimba kwa uke. Leo sitaongelea sana juu ya nini kinasababisha hizi fangasi sehemu ya uke bali tutaona dozi kamili ya asili inayoweza kutibu kabisa tatizo hili linalosumbuwa wanawake wengi miaka sasa. Tumia dawa hizi 3 zote kwa pamoja ili kupata matokeo mazuri na usiache kuleta mrejesho hapa namna unavyoendelea: 1. LEMONADE Lemonade inaandaliwa kwa kutumia limau, maji, asali na mdalasini ya unga kidogo, nayo inaandaliwa hivi: *Chukua asali mbichi nusu Lita *Chukua limau kubwa 12 au zaidi, zikate katikati kila moja. Zikamuwe moja baada ya nyingine kupata maji maji ya limau mpaka umepata ujazo wa nusu lita. *Kwenye sufuria nyingine kubwa changanya mdalasini ya unga vijiko vikubwa 10 na maji lita 2 na nusu na uchemshe kama chai kisha ipua na uchuje na usubiri ipowe iwe ya uvuguvugu kidogo. *Sasa changanya pamoja asali nusu lita, juisi au maji maji ya limau nusu lita, maji ya uvuguvugu ya m...

TIBA YA MTU ALIEINGIWA NA JINNI SUGU.

kabla sijatoa tiba yake, ni lazima ujue unatibu nini na kwanini ni jinni. Maana zipo dalili mbalimbali zinazoonyesha mgonjwa amehusudiwa na jini na ni jini aina gani aliemuingilia muhusika. Zifuatazo ni aina na utaratibu wa kumtibu jini sugu. Dawa za kula. Habbatsaudai Habbatsufa Bakahadi Manimani Uzile Habbat rehani Karkam Halilinji Alhamza Kamun aswad Zamda Khardal Daarfilfil Filfil aswad Haltit Zaatar Harmal Sufa nyeupe Manimani Shomari Udinadi Ulinjani Sakabanji Kamun abyadh Uwatu Giligilani Karafuu Tangawizi Mdalasini Maua waridi Hakikisha dawa hizi umezitwanga na kuwa laini kisha utachukua kijiko kimoja cha kila dawa na kuchanganya kwenye asali safi ya nyuki lita moja na uisomee ruqya na mgonjwa awe anakunywa vijiko viwili mara tatu kwa siku kwa mda wa siku 30. NB Hakikisha wakati mgonjwa anatumia dawa za kula ambatanishe na za kujifukiza pamoja na za kujipaka. DAWA ZA KUFUKIZA kiribiti upele Sandarusi Haltit Karafuu maiti Mruturutu ...

KICHOMI

  Kichomi   ni moja ya dalili za ugonjwa moyo. Kupatwa kichomi mara moja moja si vibaya. Ukipatwa muda mrefu au kila wakati ; basi, chunguza zaidi. Kichomi husababishwa au kinaweza kuwa. Dalili ya matatizo ya tumbo lenye asidi (acid) kuzidi Dalili za ugonjwa wa moyo uitwao Ischemic Jambo la kuangalia ni je? Unashikwa kichomi ukiwa unatembea? Umeinama au umelala Ukishakula chakula Kama unapatwa kichomi wakati ukitembea au ukishafanya mazoezi makali ina maana kuna tatizo la damu kuingia sawasawa au kuzunguka (circulation) katika moyo. Kama unapatwa kichomi baada ya kula ina maana kuna tatizo katika chakula unachokula. Je mlo wako una acid(uchachu) sana? Je, unakula vyakula vyenye pilipili na binzari(spices) kwa wingi sana? Kama una kula sana vyakula vyenye asidi ina maana tumbo lako halimeng’enyui sawasawa linachoka. Kawaida binadamu unabidi kubadili badili ulaji. Usirudie vitu fulani fulani kila siku. Mathalan usiweke pilipili katika kila mlo. Tatizo ji...