Jee, wewe ni mmojawapo wa wale wanawake wanaohisi kuwa na tatizo la uchi kulegea? Haupo peke yako, wanawake wengi wanatatizwa na jambo hili, wanaweza kuwa wameambiwa jambo hili na wapenzi wao au wao wenyewe walijaribu kujipima kwa kujiingiza vidole kwenye sehemu hizo za siri. Katika makala hii natumia neno uchi, ambalo si neno sahihi sana, nikimaanisha sehemu ya nyeti za mwanamke ambayo hutumika wakati wa kufanya mapenzi, kupitisha damu chafu wakati wa siku za hedhi na kupitisha mtoto wakati anapozaliwa. Neno sahihi ni Kuma. Nalitumia neno hilo kukudhi haja ya wengi waliolizoea. Maneno mengine ambayo yamezoeleka kueleza tatizo hilo ni uchi mpana, uchi mkubwa na mengineyo.
Dalili Za Uchi Kulegea
Kabla ya yote tutazame uchi huu ulivyoumbwa. Uchi ni kama kijimfuko kirefu kilichozungukwa na misuli ambacho kwa ndani kimezungukwa na utando laini unaovutika wenye unyevunyevu unaosaidia kupunguza msuguano na wenye uwezo wa kuleta hisia za mapenzi. Kabla mwanamke hajawa tayari kwa mapenzi, kijimfuko hiki huwa kidogo chenye urefu wa inchi 2.75 hadi inchi 3.25 na upana wa robo tatu ya inchi kule ndani kinapoishia. Baada ya kuwa tayari kufanya mapenzi, kijimfuko hiki hunyumbuka hadi kufikia urefu wa inchi 5.25 na kutanuka hadi kufikia upana wa inchi 2.5 ndani kinakoishia.
Takwimu za urefu wa uchi hazina maana sana kwetu kwa somo la leo – ni upana ndio tunaotaka kuuzungumzia. Upana huu unaweza kuongezeka kwa kulegea misuli inayouzunguka uchi au kwa kuumbwa na misuli yenye unene mdogo.
Ifahamike kuwa ni kitu cha kawaida misuli hii kulegea umri wa mwanamke unapozidi miaka 60. Sasa kama ni kweli uchi wako umelegea, utaweza kujigundua kwa kuona dalili zifuatazo:
- Kufanya tendo la ndoa hakutakupa starehe sana
- Kufanya tendo la ndoa hakutampa starehe sana mpenzi wako
- Kama utahisi kwamba hewa inaingia na kutoka kwenye uchi wako (fanny farting)
- Ukiona mkojo unavuja hasa unapocheka, kupiga chafya au kukohoa.
Sababu Za Uchi Kulegea
Kama wewe ni msichana au mwanamke ambaye hujawahi kuzaa hata mara moja, suala la wewe kuwa na uchi mpana ni la kufikirika, uwezekano ni mdogo mno au ni finyu. Kuna dhana iliyoenea kwamba mwanamke anayeshiriki ngono sana atakuwa na uchi uliolegea – Huu ni Upuuzi kabisa! Mwanamke hata akifanya ngono kiasi gani, uchi hauwezi kuwa mpana eti kwa sababu hiyo.
Sababu kubwa ya kuwa na uchi uliolegea kwa mwanamke ni tendo la Uzazi. Mwanamke anapozaa misuli inayozunguka uchi na vitu vyote vinavyoshikilia kuta za uchi huo huathirika na kupungua nguvu kwa kiasi fulani. Hivyo basi, kila unapozaa, ndivyo unavyoiathiri misuli yako zaidi. Mwanamke mwenye watoto wengi sana, uchi wake utakuwa umeathirika zaidi. Namna ulivyozaa pia inaweza kuchangia, kwa mfano kuzaa kwa matatizo (Plonged labours).
Comments
Post a Comment