Skip to main content

Posts

UDHAIFU WA MBEGU ZA KIUME

Kama kila ukifanya tendo la ndoa, mwanamke anatoka shahawa/mbegu dakika chache mara baada ya kumaliza tendo la ndoa hata kama hajasimama. Iyo ni dalili mojawapo mbegu za kiume sio bora - soma hadi mwisho mada hii nzuri ili kujua kiundani na suluhisho. UBORA WA MBEGU ZA KIUME (SPERM ANALYSIS). Kawaida kazi ya kiuchunguzi wa UBORA WA MBEGU ZA KIUME hufanyika katika hospitali ambapo mbegu zako za kiume huchukuliwa na kisha kuchunguzwa na daktari mzoefu. Unaweza fanya tendo la ndoa kila siku za hatari na bado usitungishe mimba. Tatizo linaweza kuwa kwa mama au baba au wote wawili.Tumesha yaelezea sana matatizo haya katika mada nyingi ziilizopita hapahapa. Kwa upande wa baba kuna wakati unaweza JITAMBUA KAMA huna mbegu bora kutokana na muonekano wa manii/shahawa zako pamoja na kiasi cha shahawa kinachotoka katika kila tendo moja. SOMA HAPA ILI UJIFUNZE MACHACHE. 1.UWINGI WA MBEGU ZA KIUME: Mbegu za kiume katika kila tendo kamilifu moja linalofanywa zinatakiwa zis...

ASTHMA/PUMU

Leo nataka kutoa tiba ya ASTHMA/PUMU. Tiba hii unaweza kujifanyia wewe mwenyewe. Chukua tembe tano za karafuu na utie kwenye sufuria yenye maji kikombe kimoja, chemsha mpaka ibaki nusu kikombe. Kisha chuja na utie asali safi kijiko kimoja baada ya kupoa. Baada ya hapo kunywa yote kwa mara moja. Utafanya zoezi hili mara mbili kwa siku. Inshaallah utapona.

UCHAFU UNAOTOKA UKENI

Uke wa mwanamke hufanya kazi ya kutoa njia kati ya sehemu ya nje ya mwili na viungo vya uzazi vya ndani vya mwanamke. Hali ya kawaida ya majimaji yaliyomo katika uke wa mwanamke huwa ni ya tindikali ili kuzuia maambukizi ya vijidudu wa kuleta maradhi. Hali hii ya utindikali huletwa na bacteria waishio katika uke wa mwanamke. Bacteria hawa ni wa kawaida na hawana madhara kwa mwili. Uke ulio katika hali nzuri hutoa majimaji haya ili kujisafisha. Majimaji haya yanayotengenezwa katika uke na kwenye eno la cervix hufanya kazi ya kuondoa seli zilizokufa na bacteria waharibifu nje ya mwili na huu ndio uchafu wa kawaida ambao mwanamke hutoa ukeni. Kutoa uchafu huu sehemu za siri ni njia ya kuusafisha uke na kuzuia maambukizi ya magonjwa. Kitu cho chote ambacho kitaharibu uwiano wa utengeneaji wa majimaji haya ndani ya uke kinaweza kujenga mazingira ya maambukizi katika uke. Uchafu Wa Sehemu Za Siri Ulio Wa Kawaida Wanawake wote hutoa uchafu sehemu za s...

UCHI KULEGEA

Jee, wewe ni mmojawapo wa wale wanawake wanaohisi kuwa na tatizo la uchi kulegea? Haupo peke yako, wanawake wengi wanatatizwa na jambo hili, wanaweza kuwa wameambiwa jambo hili na wapenzi wao au wao wenyewe walijaribu kujipima kwa kujiingiza vidole kwenye sehemu hizo za siri. Katika makala hii natumia neno uchi, ambalo si neno sahihi sana, nikimaanisha sehemu ya nyeti za mwanamke ambayo hutumika wakati wa kufanya mapenzi, kupitisha damu chafu wakati wa siku za hedhi na kupitisha mtoto wakati anapozaliwa. Neno sahihi ni Kuma. Nalitumia neno hilo kukudhi haja ya wengi waliolizoea. Maneno mengine ambayo yamezoeleka kueleza tatizo hilo ni uchi mpana, uchi mkubwa na mengineyo. Dalili Za Uchi Kulegea Kabla ya yote tutazame uchi huu ulivyoumbwa. Uchi ni kama kijimfuko kirefu kilichozungukwa na misuli ambacho kwa ndani kimezungukwa na utando laini unaovutika wenye unyevunyevu unaosaidia kupunguza msuguano na wenye uwezo wa kuleta hisia za mapenz...
KUNG'ARISHA USO NA KUTOA MADOA DOA USONI. Chukua uwatu usage mpaka uwe laini sana. Kisha utaosha uso wako kwa maji vuguvugu na ukaushe kabisa. Baada ya hapo utachukua unga wa uwatu kijiko kimoja na utachanganya maji ya kawaida ama maji ya waridi mpaka iwe marham/rojo (paste) na utajipaka usoni na kuiacha ikauke kwa mda wa dakika 10-15 na utaosha na kupaka mafuta yako. NB Hakikisha zoezi hili unalifanya mara tatu kwa wiki kwa ajili ya matokeo mazuri. Na ni bora ukifanya usiku kabla hujalala.
NAMNA YA KUTENGENEZA SIKI YA APPLE. Mahitaji - apple mbili - Kopo lililo na mfuniko. - sukari - maji Matayarishi Unachukua apple unazikatakata vipande vidogo vidogo, kisha unavitia ndani ya lile kopo kisha unatia maji kwenye lile kopo na kuweka sukari hakikisha glass moja ya maji kwa sukari kijiko kimoja, tia maji kwenye kopo Baada ya hapo funika na na uhifadhi sehemu salama. Hakikisha unakoroga kila baada ya siku kadhaa. Utaacha kwa mda wa siku 14. Kisha chuja na hifadhi kwenye friji ili ikae mda mrefu. Baada ya mda kuisha itakuwa siki tayari na unaweza kuijaribu kwa kuionja ama kusikiliza harufu yake. Siki mara nyingi inatumiwa kama dawa, kiungo katika kupikia ama kusafishia vyombo.

MOYO KUPANUKA

Moyo kupanuka au kuwa mkubwa ni tatizo ambalo huathiri utendaji wa mfumo wa usambazaji damu mwilini. Ni hali inayosababishwa na ukinzani wa moyo jinsi unavyotoa na kuingiza damu katika mishipa ya moyo na kuelekea sehemu mbalimbali za mwili. Moyo kupanuka kutokana na kutokana na mazingira ya kusukuma damu kwa nguvu ya ziada tofauti na kawaida, hivyo kusababisha misuli ya moyo kuharibika. Wakati mwingine moyo hutanuka bila sababu zinazojulikana moja kwa moja. Pia, wakati mwingine moyo unaweza kutanuka kwa kipindi kifupi kutokana na mgandamizo kwenye mwili wako mfano ujauzito. Hali nyingine ni tatizo la moyo ulilozaliwa nalo, kuharibika kwa moyo kutokana na mshtuko wa moyo, kudhoofu kwa misuli ya moyo au moyo kutodunda kwa mpangilio. Mazingira hayo huweza kusababisha moyo kutanuka. Hali zingine za kiafya zinazohusiana na moyo kutanuka ni kama zifuatazo: Kupanda kwa shinikizo la damu Hali hii husababisha moyo kusukuma damu kwa nguvu zaidi ili kuifikisha sehe...