Skip to main content

Posts

MDUDU WA KIDOLE

Huu ni ugonjwa unaoathiri vidole vya miguu na mikono, sana sana unaathiri mikononi nadra sana mguuni.tatizo hili lisipotibiwa kwa mapema linaweza hata kufanya kidole kikakatika. Zifuatazo ni tiba za kutibu maradhi Haya :-  Njia ya kwanza Chukua mbaazi kidogo kisha ziroweke kwenye maji kwa mda mpaka zilainike, halafu utaziweka kwenye kinu na kuzitwanga mpaka zilainike, ukikosa kinu tumia kitu chochote cha kusagia ili tu ziwelaini sana. Halafu utachukua dawa hiyo na kupaka kwenye sehemu iliyoathirika na kufunga kwa kitambaa usiku mzima. Na ukiamka itakuwa imechuja uchafu wote na kufanya sehemu iliyoathirika kupona, ikiwa bado toa hiyo dawa na kufunga nyengine. Kwa uwezo was ALLAH dawa hii utapona na no mujarrab. Njia ya pili Tiba hii ni kwa mdudu anaeanza sasa kabla hajaiva na kuwa rangi ya njano. Chukua kitunguu thaum kisage kiwe laini na upake sehemu iliyoathirika kwa mda was masaa 12 kisha toa na kupaka nyengine mpaka utakapo pata nafuu. Mpemba herbal +254732917064...

HEDHI KUTOKA KIDOGO KIDOGO.

hii Mara nyingi inasababishwa na mambo kadhaa ikiwemo hormone imbalance, kutumia Dawa za family planning na matatizo mbali mbali yanayompata mwanamke ndani ya mwezi uliopita. Kwa ushauri mwanamke anatakikana spate vipimo ama amuone daktari kwa vipimo na ushauri zaidi. Kama itakuwa sio kwababu ya mimba basi mgonjwa anatakikana kutumia Dawa zifuatazo ilikufanya hedhi itoke kama kawaida. 1. Chukua mvuje na pilipili manga chemsha pomoja na anywe kikombe cha kahawa kutwa Mara tatu. 2. Chukua manemane ichemshe na mgonjwa anywe asubuhi kabla ya kula kitu kwa mda wa siku tatu. Kwa Dawa na ushauri wa magonjwa mengine wasiliana nami +254732917064.

SARATANI YA NGOZI (MELANOMA )

Melanoma ni saratani hatari sana kwa maisha ya mwanadamu. Saratani hii huwapata watu wachache lakini inapotokea mtu akapata saratani hii basi maisha yake huwa hatarini. Saratani hii si rahisi kugundulika ikilinganishwa na saratani nyingine za ngozi. Siyo tu kwamba saratani hii ni ngumu kidogo kutambulika bali pia husambaa haraka zaidi kuliko saratani nyingine za ngozi. Melanoma huweza kusambaa na kushambulia viungo vingine zaidi ya ngozi kama mifupa na ubongo. Inapofikia hatua hii saratani hii huwa ngumu sana kutibika. Ni nani wanaoweza kupata kansa ya ngozi? Mbali na watu ambao wamewahi kupigwa na jua kwa muda mrefu sana, au wale wanaojianika juani kwa vipindi virefu, wale walio na ngozi nyeupe, nywele na macho ya rangi hafifu, wenye mabaka na madoadoa, na wale ambao mtu fulani katika familia yao amekuwa na ugonjwa huo, wanaweza kuupata. Watu weupe hupatwa na kansa ya ngozi zaidi kuliko watu weusi. Lakini je, hii inamaanisha kwamba kadiri ngozi yako inavyounguzwa na jua na kuwa n...

KUVIMBA MWILI

Assalamu alaikum  Kwa mtu mwenye tatizo kama hili anatakiwa achukue kamun (bizari ile inayopikiwa pilau ) na karawiya kiingereza inaitwa caraway. Hakikisha kila moja ni ujazo sawa na ponda iwe unga laini. Kisha tia kijiko kimoja cha unga huo kwa Maji vuguvugu glass moja na unywe yote. Hakikisha unakunywa asubuhi kabla hajakula kitu kwa mda wa siku 30. In shaa llah utapona. Kwa tiba ya aina yeyote wasiliana nami.

KUVIMBA MIGUU KWA MJAMZITO.

Akina mama wengi huwa wanapata matatizo ya kuvimba miguu wakati wa ujauzito kwa sababu mbalimbali. Wengine huwa ni kawaida kwa maana ya kwamba haisababishwi na ugonjwa wa aina yoyote. Wakati mimba inapokua kubwa huweza tumbo la uzazi Uterus hukandamiza mishipa ya damu inayorudisha damu kwenye moyo Veins au ile mishipa inayobeba maji damu lymph kutoka kwenye miguu. Hali hiyo hufanya damu na hayo maji damu kushindwa kurudi yote kwenye moyo na kujikusanya sehemu ambazo ni Dependent hasa miguuni na kusababisha uvimbaji wa miguu Dependent Oedema. Uvimbaji huu ni ule ambao sana uko kwenye sehemu ya mguu chini ya kifundo cha mguu Ankle Oedema, kama miguu ikivimba kupanda juu hadi kwenye mapaja au juu zaidi hii huwa ni dalili ya ugonjwa. Magonjwa ambayo yanaweza kusababisha uvimbe miguuni na sehemu nyingine za mwili wa mjamzito ni pamoja na kuwa na shinikizo la damu la ujauzito Pre-eclampsia, magonjwa ya figo ambapo mtu huvimba miguu, uso pia, magojwa ya ini – haya husababisha p...

TIBA YA ASILI YA FANGASI UKENI.

Fangasi ukeni ni muwasho sehemu ya ndani ya uke ambao unaweza kuambatana pia na kuvimba kwa uke. Leo sitaongelea sana juu ya nini kinasababisha hizi fangasi sehemu ya uke bali tutaona dozi kamili ya asili inayoweza kutibu kabisa tatizo hili linalosumbuwa wanawake wengi miaka sasa. Tumia dawa hizi 3 zote kwa pamoja ili kupata matokeo mazuri na usiache kuleta mrejesho hapa namna unavyoendelea: 1. LEMONADE Lemonade inaandaliwa kwa kutumia limau, maji, asali na mdalasini ya unga kidogo, nayo inaandaliwa hivi: *Chukua asali mbichi nusu Lita *Chukua limau kubwa 12 au zaidi, zikate katikati kila moja. Zikamuwe moja baada ya nyingine kupata maji maji ya limau mpaka umepata ujazo wa nusu lita. *Kwenye sufuria nyingine kubwa changanya mdalasini ya unga vijiko vikubwa 10 na maji lita 2 na nusu na uchemshe kama chai kisha ipua na uchuje na usubiri ipowe iwe ya uvuguvugu kidogo. *Sasa changanya pamoja asali nusu lita, juisi au maji maji ya limau nusu lita, maji ya uvuguvugu ya m...

BUNSAJI

Leo nataka kupeana faida ndogo kuhusu mafuta yaliyochanganywa na *BUNSAJI.*mafuta haya hufaa sana kwa :- - kichwa kilicho na harara ukipaka kichwani. - mafuta hayo huwafaa sana watu ambao hawapati usingizi wakipaka kichwani. - mafuta hayo hurutubisha ubongo ukipaka kichwani. - hufaa sana kwa watu wenye uyabisi na kupasuka pasuka ( dandruff ) ukipaka kichwani. -  hufaa sana kwa mtu anaejikuna sana kichwani.  *NAMNA YA KUYATENGENEZA.* chukua bunsaji kisha iponde iwe unga kisha iroweke katika maji unayotaka kuyachemsha masaa 12, baada ya hapo utaichemsha sana mpaka ibaki sawa na mafuta yako unayotaka kuchanganyia kama ni ya nazi, zaituni ama yeyote yale. Kama itakuwa mafuta yako ni nusu lita hakikisha umeichemsha bunsaji mpaka ikafika nusu lita nayo, kisha changanya pamoja baada ya kuichuja na uweke jikoni ichemke mpaka maji yote ya bunsaji yamekauka na kubaki mafuta pekee. Hapo sasa itakuwa tayari kwa matumizi. Kwa ushauri/tiba ya maradhi mbalimbali wasiliana nami.