Skip to main content

BAWASILI

Hiki ni kinyama kinachotoka ndani ama nje ya tupu kubwa. Kinapotoka nje huitwa bawasili ya nje na kikitoka ndani nayo itakuwa kinyume chake. Zifuatazo ni baadhi ya tiba za bawasili.

Bawasili ya nje
Chukua mafuta ya mbono na upake sehemu ilipotoka na uingize ndani. Baada ya kuingiza ndani utachukua dawa zifuatazo na ujifukize .
- haltit
- kiribiti upele
- shubiri nyeusi
- kamun aswad
- kuzbara
- mvuje
- majani ya toto la yaliyoanguka yenyewe na uyakate vipande vidogovidogo.

Na mgonjwa atachanya zote na kujifukiza sehemu ya haja kubwa mara tatu kwa siku.

Na kama itakuwa ni ya ndani ama ya nje mgonjwa anaweza chukua dawa inayoitwa MAKALARZAK na kuchemsha kisha anywe nusu kikombe kutwa mara tatu mpaka atakapo pata nufuu.

Popular posts from this blog

MDUDU WA KIDOLE

Huu ni ugonjwa unaoathiri vidole vya miguu na mikono, sana sana unaathiri mikononi nadra sana mguuni.tatizo hili lisipotibiwa kwa mapema linaweza hata kufanya kidole kikakatika. Zifuatazo ni tiba za kutibu maradhi Haya :-  Njia ya kwanza Chukua mbaazi kidogo kisha ziroweke kwenye maji kwa mda mpaka zilainike, halafu utaziweka kwenye kinu na kuzitwanga mpaka zilainike, ukikosa kinu tumia kitu chochote cha kusagia ili tu ziwelaini sana. Halafu utachukua dawa hiyo na kupaka kwenye sehemu iliyoathirika na kufunga kwa kitambaa usiku mzima. Na ukiamka itakuwa imechuja uchafu wote na kufanya sehemu iliyoathirika kupona, ikiwa bado toa hiyo dawa na kufunga nyengine. Kwa uwezo was ALLAH dawa hii utapona na no mujarrab. Njia ya pili Tiba hii ni kwa mdudu anaeanza sasa kabla hajaiva na kuwa rangi ya njano. Chukua kitunguu thaum kisage kiwe laini na upake sehemu iliyoathirika kwa mda was masaa 12 kisha toa na kupaka nyengine mpaka utakapo pata nafuu. Mpemba herbal +254732917064...

UTOSI KUINGIA NDANI KWA MTOTO MCHANGA.

chukua manjano mbichi iponde iwe laini sana, kisha chukua pamba na uiweke ile dawa, kisha muekee mtoto mchanga aliena tatizo hilo utosini. In shaa allah utosi utarudi sawa. Utafanya hivyo kwa siku mara moja mpaka tatizo litakapokwisha.

HEDHI KUTOKA KIDOGO KIDOGO.

hii Mara nyingi inasababishwa na mambo kadhaa ikiwemo hormone imbalance, kutumia Dawa za family planning na matatizo mbali mbali yanayompata mwanamke ndani ya mwezi uliopita. Kwa ushauri mwanamke anatakikana spate vipimo ama amuone daktari kwa vipimo na ushauri zaidi. Kama itakuwa sio kwababu ya mimba basi mgonjwa anatakikana kutumia Dawa zifuatazo ilikufanya hedhi itoke kama kawaida. 1. Chukua mvuje na pilipili manga chemsha pomoja na anywe kikombe cha kahawa kutwa Mara tatu. 2. Chukua manemane ichemshe na mgonjwa anywe asubuhi kabla ya kula kitu kwa mda wa siku tatu. Kwa Dawa na ushauri wa magonjwa mengine wasiliana nami +254732917064.